Rwanda yatangaza imepata mafuta katika ziwa Kivu

Farmland on steep hillside near Lake Kivu, Rwanda

Cultivated farmland covers the rugged hills of Rwanda near Lake Kivu Source: Moment RF / by Marc Guitard/Getty Images

Rwanda imesema Jumatano kuwa imefanya ugunduzi wa mafuta katika Ziwa Kivu, ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika nchi isiyo na bahari katika eneo la Maziwa Makuu, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.


Francis Kamanzi, mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Madini, Mafuta na Gesi nchini Rwanda, amekiambia kikao cha bunge cha taifa, kama ilivyonukuliwa na vyombo kadhaa vya habari, ikiwa ni pamoja na tovuti ya habari ya Igihe.

Bw.Kamanzi amesema kuwa visima 13 vya uchunguzi vilivyochimbwa upande wa Rwanda wa Ziwa Kivu, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), vinaonyesha uwepo wa mafuta.

Kaskazini zaidi, amana kubwa tayari zimegunduliwa nchini Uganda, katika eneo la Ziwa Albert, amekumbusha, akisisitiza kwamba mafuta hayo yaliyogunduliwa yako katika sehemu sawa ya Bonde la Ufa na Ziwa Kivu.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share