Wasafiri wana onywa wabaki nyumbani kama wanaweza kwa sababu ya dhoruba na hatua zanazo endelea zakiviwanda zinazo tumbukiza mfumo wa reli wenye shughuli nyingi zaidi nchini Australia katika hali ya machafuko. Takriban nusu ya huduma zote za reli za New South Wales zilifutwa Jumatano wakati, chama cha wafanyakazi wa Reli, Tram na Basi kili rejesha marufuku yakufanya kazi wakati kikishauriana na serikali ya jimbo kuhusu toleo jipya la malipo.
Rwanda imesema Jumatano kuwa imefanya ugunduzi wa mafuta katika Ziwa Kivu, ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika nchi isiyo na bahari katika eneo la Maziwa Makuu, kulingana na vyombo vya habari vya ndani. "Habari njema ni kwamba tuna mafuta," Francis Kamanzi, mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Madini, Mafuta na Gesi nchini Rwanda, amekiambia kikao cha bunge, kama ilivyonukuliwa na vyombo kadhaa vya habari, ikiwa ni pamoja na tovuti ya habari ya Igihe. Bw.Kamanzi amesema kuwa visima 13 vya uchunguzi vilivyochimbwa upande wa Rwanda wa Ziwa Kivu, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), vinaonyesha uwepo wa mafuta.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili