Key Points
- Australia Day marks the day the British raised the Union Jack flag in Sydney Cove in 1788, which was the start of colonisation.
- January 26 marks the beginning of British colonisation, a painful part of Aboriginal and Torres Strait Islander history.
- Polls show a majority of Australians want Australia Day to remain on January 26.
Januari 26 ni siku kuu rasmi ya Australia. Ila kwa watu wa Asili na, kwa wa Australia wengi hii si siku yaku sherehekea.
Boe Spearim, ni mwanaharakati mwenye asili ya Gamilaraay, Kooma, na Murrawari, yeye pia hutengeza makala yaliyo rekodiwa, ana elezea uzoti wakihisia wa siku hiyo.
“Kwangu, ninapo fika katika siku hiyo, asubui, huwa na hisi nikama naenda kwa mazishi. Najua kitu kibaya kimefanyika. Ni hisia mbaya sana.”
Kwa nini Siku Kuu ya Australia huwa Januari 26
Januari 26, 1788, Wangereza wali inua bendera yao katika eneo la Sydney Cove, hatua iliyo ashiria mwanzo wa ukoloni.
Siku kuu ya Australia ime adhimishwa Januari 26 tangu 1935 ila, ilikuwa likizo ya umma kitaifa katika mwaka wa 1994.
Baadhi yawa Australia husherehekea kwaku choma nyama nama rafiki pamoja na familia, kwenda fukweni au kutazama fataki. Sherehe nyingi za uraia hufanywa pia siku hiyo.
Ila Januari 26 imechukuliwa kama "Siku ya maombolezi" nawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait tangu 1938. Idadi kubwa yawa Australia hukataa kusherehekea siku hiyo na wanaomba likizo hiyo yakitaifa ihamishwe katika tarehe tofauti.
Invasion Day Rally in Brisbane, 2024 Source: AAP / JONO SEARLE
Kwa nini nisiku ya huzuni kwa wa Australia wa Asili?
Dkt Summer May Finlay, ni mwanamke wa ukoo wa Yorta Yorta, yeye pia ni mhadhiri mkuu katika chuo cha Wollongong, ame elezea kuwa Januari 26 inawakilisha mwanzo wa mateso kwa wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait.
“Ni mwanzo wa ubaguzi wa rangi, ni mwanzo wa ubaguzi, ni mwanzo wa wakati ambapo watu wetu walinyimwa haki kutoka jumuiya na nchi ambayo mababu zetu walitembea kwa zaidi ya miaka elfu 65.”
Ukoloni wa Uingereza umekuwa na madhara kwa wa Australia wa Asili, ambao walikabiliwa kwa kunyang'anywa ardhi, kuuawa, kuletewa magonjwa pamoja na watoto kuondolewa kwa nguvu.
Madhara ya ukoloni, yanajumuisha ubaguzi wakimfumo, matokeo mabaya ya afya na uwakilishi mkubwa katika mfumo wa haki, una hisika bado hadi leo.
Dkt Finlay amewahamasisha wa Australia wote, wajifunze kuhusu historia ya nchi yao.
“Nadhani Australia ni nchi nzuri katika hali nyingi. Nina uhakika watu wanao kuja nchini humu na ni raia wapya, wata kiri nakutambua hilo. Ila wakati huo huo, tuna historia katika nchi hii ambayo si nzuri na haija tambuliwa haswa.”
Badilisha, kubali au futa tarehe?
Tafiti zina onesha kuwa . Ila, kila mwaka, watu wengi wanataka tarehe hiyo ya siku kuu ya taifa ibadilishwe.
Wa Australia wengi wa Asili wanataka tarehe hiyo ibadilishwe, ingawa baadhi yao wanaweka kipaumbele kwa kutambuliwa kwa historia yake juu yaku ibadilisha. Wengine kama Boe Spearim, wana amini siku hiyo inastahili futwa kabisa.
“Ina husu kufuta uelewa waki koloni kuwa nchi hii ili chukuliwa kwa amani au kuwa, kilicho fanyika kwa watu waki Aboriginal hawastahili tambuliwa, wakati inastahili. Na inahusu kuwakumbusha wabaguzi wa rangi na umma mpana kuwa hauwezi sherehekea mauaji ya kimbari tena, si sawa,” amesema.
People gather outside Victorian Parliament for the Invasion Day rally, 2024. Source: AAP / Diego Fedele
Jinsi yaku adhimisha kwa heshima Januari 26
Makundi yawatu waki Asili huandaa maandamano, mikutano ya hadhara, ibada za alfajiri pamoja na matukio yakitamaduni kote nchini siku ya Januari 26, wakitambua siku hiyo kama "siku ya uvamizi" au "siku yakuokoka”.
Dkt Finlay ana elezea jinsi siku hiyo huwa na nani anaweza shiriki.
“Maandamano huwa ya amani katika mitaaa. Nilishiriki katika maandamano kadhaa nilipokuwa niki ishi Melbourne. Na ni njia nzuri kwa familia kuja pamoja, iwapo niwa Aboriginal na familia zawana visiwa wa Torres Strait, au hata familia zisizo zawatu wakiasili.”
Rana Hussain ni mwanachama wa bodi ya shirika la Reconciliation Australia, hilo ni shirika lisilo la faida linalo kuza maridhiano kati yawa Australia wakiasili na wasio wakiasili. Amesema mikusanyiko hii hutoa matumaini na umoja.
“unapata hali hiyo ya ushikamano na mara nyingi huwa unapata ile hali ya matumaini kuwa pamoja na jumuiya. Kama washirika, nadhani ni muhimu tusimame nyuma yawa Australia wa kwanza, wanapo fanya harakati yakubadilisha tarehe au, kutambua zaidi maana ya siku hii kwao.”
Halmashauri kadhaa za jiji hazifanyi tena matukio ya Siku kuu ya Australia, pamoja na sherehe za uraia Januari 26. Baadhi ya sehemu za kazi huwa ruhusu wafanyakazi kubadilisha siku hiyo ya likizo na siku nyingine.
New Australian citizens, Broken Hill, NSW Source: AAP / STUART WALMSLEY
Ni wahamiaji wangapi wanaweza husiana nawa Australia wa Asili
Bw Spearim ana amini wahamiaji, wengi ambao wamepitia uzoefu wa vita, makwao kutekwa wanaweza, kuwa na huruma harakati zawatu waki Asili.
“Ni ajabu kuwa watu huja hapa nakupata aina fulani ya amani. Tangu 26 Januari 1788, hatuja pata haki, hatuja pata amani,” amesema.
Rana Hussain naye amesema kuwa swala la Januari 26, linastahili kuwa muhimu kwa Australia wote, situ watu wa Asili.
“Nadhani watu wengi, wanafikiria kuwa hali hii ngumu na huzuni pamoja na huzuni niya watu wa mataifa ya kwanza pekee ila, hakuna anaye elewa umuhimu wa siku hiyo anaweza hisi uchungu kuhusu hili. Na kwangu, kuwa mtoto wa wahamiaji wahindi, tuna historia yetu binafsi ya ukoloni na ukoloni wa Uingereza.”
Kama mhamiaji wa kizazi cha pili, Bi Hussain ana elewa kwa nini wahamiaji wengi wanataka sherehekea utambulisho wao mpya.
Ila ana amini wa Australia wote wanastahili kuwa na mazungumzo muhimu kuhusu historia ya kweli ya nchi yetu kwa sababu tunaweza pata njia jumuishi yaku isherehekea.
“Nadhani tunastahili kuwa na mazungumzo hayo kama nchi, kisha tunaweza zungumza kuhusu siku tunayo taka sherehekea historia hiyo yote nakutambua historia hiyo kisha tunakuja pamoja. Unajua, ni siku gani inastahili tu unganisha sote.”
Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia yafafanuliwa, kwa taarifa ya muhimu na vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una maswali au wazo la mada? tutumie barua pepe kwenye anwani hii