Ongezeko ya karo ya shule yafanya familia zi hisi shinikizo

Boys at Brisbane private school

Source: AAP

Kuna salia wiki chache kwa mwaka wa shule wa 2025 kuanza, janga la gharama ya maisha lina endelea kuweka shinikizo kwa familia zinazo lipa karo ya shule.


Sasa, utafiti mpya umefichua ambako baadhi ya sehemu ghali zakusomea nchini Australia zilipo na ambako familia zinaweza mudu.

Na shinikizo hizo hazipo tu kwa familia hiyo. Katika miaka 13 ya elimu, gharama wastan yakumtuma mtoto katika shule ya serikali katika miji mikubwa ime ongezeka kwa asilimia 30, nakuzidi $123,000.

Shule huru nazo zime shuhudia gharama wastan ziki ongezeka kwa asilimia 10 nakupita zaidi ya $350,000... hata hivyo gharama ya shule zawa Katoliki ilipungua kwa chini ya asilimia 1, hadi chini ya $194.000 kulinganisha na mwaka jana.

Maeneo ya kanda na vijijini nayo pia yali shuhudia kupungua kwa gharama. Maeneo ghali zaidi kwa elimu ya shule za serikali na shule huru ni mjini Sydney, wakati kwa shule za katoliki ni mjini Canberra ambako karo ni takriban (($215,633)).

Share