Bi Wong alihudhuria hafla yakiapo cha Bw Trump na kesho Jumatano anatarajiwa kukutana na Marco Rubio, anaye tarajiwa kuidhinishwa kuwa waziri wa maswala yakigeni wa marekani katika serikali ya Bw Trump.
Wakati serikali za shirikisho nama jimbo zina endelea kufanyia kazi swala la upatikanaji wa nyumba za bei nafuu, utafiti mpya ume onesha gharama za ujenzi ni kizuizi kikubwa chakujenga nyumba nyingi zaidi. Ripoti ya CoreLogic Cordell Construction Cost Index, imeonesha gharama zakujenga nyumba ili ongezeka kwa asilimia 3.4 katika mwaka uliopita.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, aliyetekwa nyara, kwa mujibu wa mkewe, mwezi Novemba mwaka jana wakati akisafiri nchini Kenya, kwa sasa anashitakiwa mbele ya mahakama ya kijeshi, kesi ambayo wafuasi wake wanashtumu kuwa ni ujanja wa kisiasa. Anakabiliwa na hukumu ya kifo kwa uhaini na sasa yuko katika kifungo cha upweke.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amethibitisha leo Jumatatu kuzuka kwa ugonjwa wa Marburg baada ya mtu mmoja kugundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo katika wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera. Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, jijini Dar es Salaam.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.