Jeshi la polisi la Kenya lakanusha kuhusika na utekaji wa wakosoaji wa serikali

Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya Douglas Kanja, akiwa pamoja na viongozi wenzake

Jeshi la polisi Kenya limekanusha kuhusika na visa vya karibuni vya utekaji unaowalenga wakosoaji wa serikali. Watu 74 walitekwa tangu maandamano ya kuipinga serikali, huku 26 wakiwa bado hawajulikani waliko.


Vikosi vya usalama Kenya vimetuhumiwa na mashirika kadhaa ya haki za binaadamu kwa kuwateka na kuwaweka kizuizini kinyume cha sheria watu kadhaa tangu maandamano makubwa ya kuipinga serikali ya Juni na Julai mwaka huu.

Mkuu wa polisi nchini Kenya Douglas Kanja, amesema katika taarifa kuwa jeshi la polisi limeshtushwa na madai yanayoendelea kwamba maafisa wa polisi, wanahusika na utekaji wa watu nchini humo.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Share