Vita vya Australia vilikuwa vigani na kwa nini historia haivitambui?

AusWars_16x9.jpg

The Australian Wars documentary Credit: Blackfella Films

The Frontier Wars ni neno linalo tumiwa kuelezea zaidi ya miaka 100 ya migogoro ya vurugu kati ya wakoloni nawatu wa asili wa Australia, vilivyo tokea wakati wangereza walikuwa wakianza kuishi Australia. Hata kama Australia ni taifa linalo enzi kushiriki kwalo katika vita ng’ambo, bado haija tambua vita vilivyo ifanya kuwa nchi iliyopo leo.


Key Points
  • The Australian Wars could only be acknowledged after the proclamation of ‘Terra Nullius’ was legally challenged and overturned.
  • The Australian wars were fought throughout the continent, from the arrival of the first fleet in 1788, and until the mid-1930s.
  • Colonial records and archaeological evidence uncovered by teams of experts demonstrate the horrific scale of the conflict.
Onyo la maudhui: Makala haya yana marejeleo ya vurugu ambayo yanaweza kera baadhi ya wasikilizaji.

Wakati katika fukwe ya taifa linalo julikana sasa kama Australia, alitangaza nchi hii kuwa ni 'Terra Nullius', maana yake ikiwa ni si ardhi ya mtu yeyote. Hata hivyo, bara hili la kisiwa lilikuwa nyumbani kwa mamia ya mataifa tofauti yawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, mamia yama elfu yawatu wa asili ambao tamko moja lili wafanya kuwa ‘chini ya utawala’ wa Uingereza.

Hali hiyo ilikuwa kichocheo cha , migogoro mibaya kati yawatu wa asili na wazungu walio kuja kuishi nchini nakuanzisha msingi wa Australia. Ila sasa historia hiyo mbaya ina anza tambuliwa.

ni mwanamke wa ukoo wa Arrernte na Kalkadoon mwenye asili pia la Ulaya. Alitengeneza filamu kwa jina la “The Australian Wars”, filamu hiyo iliweka wazi hali ya mapambano yawatu wa asili walio tetea ardhi yao kutoka kwa wangereza walio kuja kuishi huku.
These were the wars that were fought in Australia, and they were the wars that really made the modern Australian state.
Rachel Perkins, Filmmaker.
vilipiganwa katika bara nzima, kutokea wakati meli ya kwanza ya wazungu ilipo wasili katika mwaka wa 1788, hadi katikati ya ya miaka ya 1930, ila migogoro hii haikufundisha katika shule au hata kutambuliwa kama vita hadi mwisho wa karne ya 20.

ni mmoja wa wanahistoria nchini wanao heshimiwa nchini Australia, yeye pia ni mtaalam wa vita. Alipo anza kufundisha historia katika mwaka wa 1966, watu waki Aboriginal hawakuwa wakitajwa katika vitabu vya historia.

“Ili wataja wa Aborigine mara mbili tu, na hapakuwa hata chochote katika faharisi”, alisema.

Tazama trela ya filamu ya The Australian Wars:
Prof Reynolds amesema hii ilikuwa kwa sababu Vita vya Frontier haviku chukuliwa katika kati ya karne ya 20 kama vita vikubwa, vita hivyo vili linganishwa na vita vya porini.

“Mtazamo ulikuwa ni kwamba vilikuwa vidogo sana na vilikuwa vime sambaa kuzingatiwa kuwa na uzito wa vita. Hapa kuwa sare, hapakuwa wanajeshi wakuandamana... Hapakuwa mikusanyiko mikubwa na vita katika hali ya kawaida ila isitoshe, ni wazi ilikuwa aina ya vita.”

, ni mtaalam mwingine wa Vita vya Australia, naye anakubali. Amesema dhana hiyo potofu ni matokeo ya vita vya kwanza na vya pili vya dunia, ambavyo vilibadilisha jinsi vita vilikuwa vikizingatiwa.

Hata hivyo, si kawaida kwa aina ya vita hivi vikubwa katika historia ya binadam.

“Walijua wakati huo ilikuwa vita. Hati zote zaukoloni zilizungumzia vita ila, katika karne ya 20 na 21, tumepoteza mtazamo wa hilo. Na nadhani kuna sababu zandani zakisiasa, kwa nini watu wengi hawawezi itambua kama vita,” Dr Clements ame elezea.

Sababu hizo zakisiasa zina chimbuko la mkanganyiko wakisheria kati ya tamko la ‘Terra Nullius’ na Sheria ya Uingereza. Wa Aboriginal walikuwa wame tajwa kuwa chini ya utawala wa Uingereza kwa hiyo, Himaya hainge tangaza vita dhidi yao... kufanya hivyo, ingemaanisha wanatangaza vita dhidi ya raia wao,” Rachel Perkins amesema.

“Hatahivyo, Wangereza walitumia nguvu zakijeshi kuhakikisha utawala wao wa bara hilo ulikuwa na mafanikio,” ame ongezea.
Frontier War
Frontier conflicts took place across the nation. Source: Supplied / Australian War Memorial Source: Supplied

Mabo na kubadilishwa kwa 'Terra Nullius'

Vita vya Australia viliweza tambuliwa tu baada ya tangazo la ‘Terra Nullius’ ilikabiliwa kwa changamoto yakisheria nakubadilishwa, katika mwanzo wa 1990, katika kinacho julikana kama uamuzi muhimu wa Mabo.

“Hadi wakati huo, mtazamo ulikuwa kwamba wa Aborigine hawaku miliki ardhi, kwa hiyo vita havingekuwa kuhusu udhibiti wa ardhi kwa sababu hawakuwa na hati milikiza ardhi. Baada ya 1992 na hukumu hiyo, hali ya vita ilibidi ibadilike kwa sababu ni wazi ilikuwa kuhusu aina ya maswala ambayo vita daima imekuwa kuhusu: udhibiti wa eneo,” Prof Reynolds amesema.

Dr Clements amesema kufeli kwa HImaya ya Uingereza nikutambua umiliki wa ardhi wa watu wa asili nchini Australia ni kosa lakihistoria.

“Katika moyo wa ukoloni wa Uingereza wa Australia, kulikuwa dhana potofu. Tofauti na nchi zingine zote ambazo zilikuwa chini ya ukoloni wa Uingereza, hawakutambua uhuru wa wamiliki wa jadi hapa Australia. Kwa sababu ya hiyo, hapakuwa mikataba, hapakuwa jaribio lakushauriana na wenyeji na hadi leo bado tunawakati mgumu kwa mtazamo wakisheria kuelewa haki zao za ardhi ni gani.”

Na kufeli kushauriana kulisababisha umwagaji damu mubaya.

Kumbukumbu zaukoloni pamoja na ushahidi wakiakiolojia uliofichuliwa na timu zawataalam umeonesha kiwango kibaya cha mgogoro.

pekee ina zaidi ya mabaki 400 yamababu waki Aboriginal ndani ya hazina yao, nying yazo zikionesha ushahidi wa kifo kwa kunyongwa, kukatwa kichwa pamoja na mauaji ya halaiki.

Rachel Perkins amesema wajukuu wa wahanga watakumbuka daima.
A lot of Aboriginal people have been the vessels for carrying with history. Aboriginal people have handed down the stories of what happened to them, to us, in our families. So, I grew up knowing about the massacre of my people in Queensland and I knew about the violent rape of my great grandmother, etc.
Rachel Perkins, Filmmaker.
Rachel Perkins - The Australian Wars
Rachel Perkins - The Australian Wars Credit: Dylan River/Blackfella Films

Vita vyeusi

vilikuwa vibaya sana katika migogoro ya kwanza katika historia ya Australia.

“Wakati wa Vita Vyeusi watu wengi wa Tasmania wali uawa kuliko idadi yawatu wa Tasmania walio fia Korea, Malaysia, Indonesia, Vietnam, na katika misheni zakulinda amani zikijumuishwa,” Rachel Perkins amesema katika makala ya vita vya Australia.

Dr Nicholas Clements amesema kiwango cha vurugu kutoka kutoka pande zote ilikuwa mbaya sana, mamlaka wa ukoloni na wakaaji “walijawa hofu”.

“Upinzani wa waAboriginal ulikuwa wakushangaza. Kila mtu alimjua mtu katika ulimwengu wa ukoloni aliye kuwa ame uawa au kujeruhiwa nawa Aboriginal, ambao walichoma shamba zao. Ilikuwa yakutisha sana,” amesema.
In fact, serious people were contemplating having to abandon the colony.
Dr Nicholas Clements, Australian Historian.
Ila wazungu walishinda na, karibu wa angamize watu wa asili wa Tasmania.

Mgogoro huo uliongezeka kwa sababu ya ukatili wa kijinsia.

“Kichocheo cha vurugu, kiberiti kilicho washa moto, ilikuwa ukatili wakijinsia,” Dr Clements ame ongezea.

Ubakaji wakimfumo na utekaji nyara wa wanawake waki Aboriginal, ulikuwa kawaida sana kiasi kwamba ana husisha kupona kwa baadhi ya ukoo wa waAboriginal kwa mashambulizi yakijinsia.

“Ni ajabu sana kuwa tuna wajukuu wa waAboriginal Tasmania leo kwa sababu, walikaribia angamizwa kwa vurugu,” Dr Clements amesema.
What is Native Title explainer NITV Eddie Koiki Mabo
Eddie Mabo with his legal team. Source: SBS Credit: National Museum of Australia

Kupambana na moto kwa moto

Kumaliza upinzani wa waAboriginal katika sehemu nyingi za Australia, wakoloni wali unda jeshi la polisi la watu wa Asili, jeshi lililo funzwa kusambaza hofu.

“Ulisajili wanajeshi wa asili na, uliwatumia kama jeshi. Hakuna shaka hii ilikuwa nguvu kubwa yakuvunjwa upinzani wa waAboriginal,” Profesa Reynolds amesema.

Wanaume walipewa sare, bunduki na farasi. Dr Clements ana amini wali danganywa na maafisa wazungu, ambao waliwatumia kwa ujuzi wao wa utamaduni waki Aboriginal na ujuzi wa misitu.

“Gharama iliyo chukuliwa na jeshi la polisi lawatu wa asili jimboni Queensland pekee, ilikuwa katika makumi yama elfu. Makadirio yana fika kati ya elfu 60 hadi 80.000, Naamini, ambacho kinashangaza na ina tupa wingu la maadili juu ya biashara yote mbaya,” amesema.
Australian Aboriginal camp in the nineteenth century
A nineteenth century engraving of an aboriginal camp - Marmocchi Source: Getty Source: Getty
Rachel Perkins ilinibidi ni kabiliane na historia hii wakati wakutengeneza filamu ya Vita vya Australia.

“Nilipata rekodi iliyo fanywa na bibi yangu, akizungumza kuhusu jinsi famili ya mamake ilivyo uawa, ambayo nilikuwa sijawahi sikia kabla na, nilikuwa sijawahi fika sehemu ambako ilifanyika na nilikuwa sijawahi jua ilikotokea hadi nilipotengeneza hii filamu,” amesema.

Dr Clements, ambaye watangulizi wake walikuwa wakaaji, ana amini kuwa wa Australia wote wanastahili kabili hisia za aibu nakumilika dhuluma za zamani.

“Iwapo mababu wa mtu walishiriki au la, sote ni warithi wa ardhi yawa Aboriginal, iliyo ibiwa. Kwa kima cha chini, sote tuna jukumu laku fichua historia hii, kukubali historia hii nakucheza katika mustakabali chanya wa usoni.”
Nowhere was resistance to white colonisers greater than from Tasmanian Aboriginal people, but within a generation only a few had survived the Black War.
Nowhere was resistance to white colonisers greater than from Tasmanian Aboriginal people, but within a generation only a few had survived the Black War. Source: The Conversation / Robert Dowling/National Gallery of Victoria via The Conversation Source: The Conversation / Robert Dowling/National Gallery of Victoria via The Conversation

Kwa nini historia hii hai adhimishwi?

Profesa Reynolds ana amini Australia, kama taifa linalo waenzi wanajeshi wao walifariki katika kumbukumbu ya vita vyake vingi, inastahili tambua kwa uwazi ukweli kuwa migogoro ya vita iliyotokea na imegubikwa kwa matendo ya uhalifu dhidi ya ubinadam.

“Ni aje hatuwezi kubali vita vya Australia?” ame hoji.

“Hali hiyo si hivyo Marekani, wanatambua migogoro yote [Wamarekani wa asili] rasmi ya vita. Ni wazi si hivyo nchini New Zealand, vita vya wa Maori daima vime kuwa sehemu muhimu ya historia hiyo.”

Rachel Perkins amesema sababu ya hali hiyo isiyo ya kawaida ni rahisi.

“Australia ni moja ya sehemu zakipekee duniani ambako, wakoloni hawa ondoki,” amesema.
The colonists or the settlers that came with them have remained in power, so I think that makes it a bit more difficult for the nation to acknowledge or celebrate those that defended the country because the colonial occupying force hasn’t left!
Rachel Perkins, Filmmaker.
Dr Clements ana amini kuwa ‘tusi wahi sahau’, neno ambalo hutumiwa kawaida kuwa enzi wanajeshi wa Australia walio fariki, linastahili tumiwa kwa mashujaa walio pigana dhidi ya ukoloni wa Uingereza katika ardhi zao.

“Naweza hisi fahari sana kama nchi yangu inatambua kwa ujasiri, siku zake za nyuma, makosa ya watangulizi wao na, kuahidi kwa ukamilifu kurekebisha makosa hayo, kwa uwezo wao kwa siku za usoni.… Nataka watoto wangu waende huko, katika mazingira kama ni kwa kumbukumbu zao au kama nikwa majina yao mawili, ua Aboriginal uko hapo, na unatambuliwa.”

inaweza tazamwa kupitia SBS On Demand katika lugha tano: Kichina rahisi, Kiarabu, Kichina chakitamaduni, Kivietnamu na kikorea. Makala hayo pia yanaweza patikana na maelezo ya sauti/maandishi kwa watu wenye ulemavu wakuona au kusikia.
Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza Septemba 2022.

Share