Taarifa ya Habari 14 Januari 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese amefanya mkutano wake wa kwanza wa 2025 na baraza lake la mawaziri.


Wiki iliyopita, alianza ziara ya majimbo matatu muhimu katika uchaguzi akitembelea Queensland, Wilaya ya Kaskazini pamoja na Magharibi Australia, ambako alitangaza uwekezaji wa thamani yamabilioni ya dola kwa miundombinu. Tarehe ya uchaguzi mkuu bado haija tangazwa ila, lazima uchaguzi mkuu uwe kabla ya Mei 17.

Waziri wa afya Mark Butler ametetea rekodi ya serikali kwa Medicare, kufuatia ripoti iliyo onesha kupungua kwa upatikanaji wa zahanati zinazo toa huduma ya matibabu bila malipo kote nchini. Ripoti ya orodha ya huduma za afya ya Cleanbill imesema zahanati chache zama GP, zinawahudumia wateja wanao hitaji huduma bila malipo na malipo yana endelea kuongezeka.

Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Tanzania alitekwa nyara Jumapili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, na kuachiliwa baadaye baada ya makundi ya haki za binadamu kuingilia kati kwa haraka. Maria Sarungi Tsehai kutoka shirika la kutetekea haki za wanawake na mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania amepata umaarufu mkubwa, akiwa na wafuasi milioni 1.3 kwenye mtandao wa X, lakini amelazimika kuishi uhamishoni katika miaka ya hivi karibuni.

Bonyeza hapo juu usikize makala kamili.

Share