Kukumbatia maarifa ya tiba ya asili

Debbie Watson.jpg

Traditional healer Debbie Watson

Kuelewa nakuheshimu maarifa ya tiba ya asili, inaweza kuwa muhimu kwa kutoa kutoa huduma kamili na inayo faa kitamaduni katika mazingira yakisasa ya huduma ya afya.


Key Points
  • For First Nations peoples, health is a holistic concept, a complex interplay of physical, emotional, social, and spiritual well-being.
  • Traditional medicine is a mixture of the tangible and spiritual.
  • Traditional healers inherit their knowledge and healing abilities from generation to generation.
  • Traditional medicine and modern medicine can work hand in hand and offer more culturally sensitive treatment to their issues.
Kwa wa Australia wa kwanza, afya ni zaidi ya ukosefu wa ugonjwa. Ni dhana ya kiujumla yenye sifa ya mwingiliano wa kimwili, kihisia, kijamii pamoja na maswala ya ustawi wakiroho.

Kwa hiyo, tiba yaki asili hailengi tu kutibu magonjwa yakimwili, inatafuta pia kuweka usawa kati ya vipimo mbalimbali vya ustawi.

Dr Alana Gall, ni mwanamke kutoka ukoo wa Truwulway unao patikana katika eneo la pwani ya askazini mashariki ya Lutruwita, amekuwa akipenda sana tiba ya asili tangu alipokuwa kijana.

“Nyumbani, tulikuwa tunatumia dawa mbali mbali zaki asili pamoja na, mazoea tofauti, kwa hiyo kulikuwa sherehe mbali mbali na maswala yakiroho yalikuwa sehemu kubwa ya maisha yangu.”
Dr Alana Gall.jpg
Dr Alana Gall
Yeye ni mtafiti mwenza wa baada ya masono ya udaktari katika dawa ya asili katika chuo cha Southern Cross, pia ana nyadhifa kadhaa za utetezi zikijumuisha mkurugenzi wa tiba ya asili kwa chama cha muungano wa dawa za jadi Ziada na shirikishi (TCI).

Amesema kuwa istilahi "dawa ya msituni", mara nyingi hutumiwa kwa kubadilishana na tiba yakiasili, inaweza punguza uelewa wa watu kuhusu tiba ya asili ni nini.

Watu hudhani ni kitu cha kimwili kama kupumua, au kitu dawa zakumezwa.

Hatahivyo, "dawa zetu ni zaidi ya hayo", ame elezea.

“Dawa zakitamaduni zinaweza jumuisha sherehe za uponyaji, dawa zakiroho na waponyaji wakitamaduni.”
We also see our Country, our lands, as healers as well. So we have a Country of medicine as well. But underpinning all that is what people commonly talk about now, as our ways of knowing, being and doing.
Dr Alana Gall

Waganga wakienyeji

Debbie Watson ni ngangkari au mponyaji waki Aboriginal kutoka ardhi za Pipalyatjara na Aṉangu Pitjantjatjara Yankunytjatjara (APY) za Kusini Australia.

Waponyaji wa Ngangkari husaidia kurekebisha moyo, ambayo wana ona kama sehemu muhimu ya mwili wa mwanadamu.

"Naponya watu kwa mikono yangu. Naona ndani na nahisi nishati yao na kilicho ndani yao na pia huwa na fanya kazi na moyo."

Bi Watson ame elezea kuwa kama moyo umetawanywa au ume zuiwa, inaweza sababisha maumivu, wasi wasi na dalili zingine.

"Moyo hauwezi umia," amesema.

Uwezo wakuponya watu huchangiwa kutoka kizazi kwa kingine.

Bi Watson anatoka katika mstari mrefu wa waponaji. Alijifunza ujuzi huo kutoka kwa babake alipokuwa binti mchanga.  

"Alinifunza kuwa mponyaji, mponyaji imara."
Debbie Watson 2.jpg
Debbie Watson
Bi Watson ni mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa shirika la Aṉangu Ngangkaṟi Tjutaku Aboriginal Corporation (ANTAC) , hilo ni shirika la kwanza la waponyaji waki Aboriginal wa Australia.

Shirika hilo lisilo la faida husaidia nakudumisha matendo yaliyo dumu kwa karne wakati wanatoa huduma za uponyaji kwa wa Aboriginal na watu ambao siwa Aboriginal.

Dr Francesca Panzironi ni mwanzilishi mwenza na mkurugenzi mtendaji wa ANTAC, ambaye taaluma yake ilikuwa ni katika sheria ya haki za binadama zakimataifa.

Udadisi wake kuhusu tiba yakitamaduni yawa Aboriginal na pengo katika fasihi ilimfanya msomi huyo kutoka Italia, kuingia kwa kisicho julikana.

Baada yaku ungana na ngangkaris wa Kusini Australia nakushauriana na jumuiya, Dr Panzironi alitambua mahitaji ya huduma kama hizo zipatikana kwa wote.
Dr Panzironi and Debbie Watson.jpg
From left, Dr Francesca Panzironi and Debbie Watson
People really wanted them. It wasn’t just a theory. People were feeling better, people needed them.
Dr Francesca Panzironi
Leo, ANTAC inafanya uponyaji wakitamaduni upatikane kwa urahisi kwa umma, kutoka kwa huduma za afya hadi kwa huduma zamarekebisho na taasisi zingine ambazo zina nia yaku jifunza nakupata uzoefu wayo.

Wakati uponyaji wakitamaduni hauchukui nafasi ya mfumo wa madawa yakisasa, "inaweza tumika sambamba" na kutoa matibabu zaidi nyeti yanayo zingatia maswala ya utamaduni amesema Dr Panzironi.

“Inaweza tumika sambamba”

Brett Rowling ni mjukuu wa jamii ya Bungoree na Matora, na yeye pia ni mwanakemia wa uchambuzi.

Amesema dawa zakitamaduni na dawa zaki sasa, hatakama nikama zinatofautiana, zinaweza shirikiana nakuruhusu mitazamo miwili tofauti, naya kipekee.
One, it’s our oral story, teachings and morals with the secrets, and the other side is the white fella ways of working, the data and analysis. They’re two polar opposites, but two very complementary ways.
Brett Rowling
Kwa mfano, dawa ya paracetamo imetengenezwa kwa data na ya uchambuzi ila madawa yakienyeji, ambayo yame changiwa kwa hadithi. Inaweza tumika pia kwa ufanisi ila, maoni kwa ujmla yana fanana kwa wazo moja.
Brett Rowling.jpg
Brett Rowling
“Tume enda tangu mwanzo wa wakati. Tulikuwa na kila kitu. Si kama tulikuwa tunasuburi wazungu waje kuelezea jinsi hii ina stahili tumika. Tulikuwa navyo tayari, dawa tofauti na mbinu.

Bw Rowling amesema ni wakati waku "amusha hali hiyo nakuonesha watu na dunia.”

Kuna mengi zaidi ambayo dunia inawezi faidi kupitia ujuzi huu Dr Gail amesema.

“Nchini Australia, sisi ndio tamaduni kongwe zaidi inayo endelea duniani. Kwa hiyo kuna maarifa tunayo kuhusu jinsi yaku linda dunia, jinsi yakutengeneza madawa katika mbinu ambazo tumekuwa tuki fanya tang zamani.

tuki kusanya ujuzi huo, basi tunaweza fanya mabadiliko katika matatizo ya leo. kama vile aina ya jiduu ame elezea Dr Gall.

Sayansi yaki sasa inaweza toa pia data inayo hitajika na uchambuzi kutazama usalama wa madawa yakitamaduni.

Ulinzi wa maarifa

Hata hivyo, bila ulinzi sahihi kwa maarifa haya, baadhi ya jumuiya zina sita kuchangia maarifa yao na, katika kesi mbaya, wazee huaga dunia, nakuchukua maarifa hayo nao, ame elezea Dr Gall.

“Uhalisia ni kwamba maarifa yetu hayaja lindwa. Hiyo ina maana haiko salama kwetu kutoa maarifa hayo bure.

Ameongezea kuwa kampuni zamadawa, vipodozi na ukulima zinaweza chukua maarifa hayo, kuyafanya biashara naku pata faida kubwa.

Kwa hiyo, watu wanao miliki maarifa haya hawa wezi pata nakufaidi kupitia maarifa hayo, hali ambayo inazua wasiwasi pia kuhusu uendelevu, aliongezea.

Lengo la muda mrefu la Dr Gall, niku unda mfumo ili maarifa haya yaweze changiwa kwa faida ya afya ya binadam wote duniani.

Share