Key Points
- First Nations knowledge of weather and seasons has been passed down through the generations through oral and visual storytelling and cultural traditions.
- The seasonal cycles described by First Nations peoples vary across Australia according to their geographic location.
- First Nations weather knowledge incorporates understanding of how changes in the behaviour of animals or growth of plants ties in with changes to weather and seasons.
Kuelewa hali ya hewa na misimu yake, ni kipengele cha kina cha ujuzi wakitamaduni wa wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, ambao umefanyiwa kazi kwa makumi yama elfu ya miaka.
Hali ya hewa hutengeza mizunguko ya maisha ya wanyama na mimea, na kuelewa miunganiko hii ni muhimu kwa uhai wa binadam haswa nchini Australia, ambako kukithiri kwa msimu na mandhari mbaya yana omba kuwa tayari kubadilika.
Kila kitu kina ungwa, ni falsafa muhimu ya utamaduni wa Mataifa ya Kwanza na katika milenia, watu waki Aboriginal na visiwa vya Torres Strait wa Australia, walitazama mazingira nakujifunza miunganisho ya mara kwa mara kati ya mazingira, hali ya hewa, misimu na mabadiliko kwa maisha ya wanyama na mimea wanako ishi.
Mwito wa ndege fulani unaweza ashiria ujio wa mvua na, kuchepuka kwa maua ya mmea fulani au mti, kuna weza ashiria kubadilika kwa msimu na muda waku hamia katika sehemu nyingine ya ardhi.
Shangazi Joanne Selfe ni mwanamke kutoka jamii ya Gadigal [Gad-e-gal], inayo patikana katika pembe ya mashariki ya Australia. Alikuwa aki jifunza kuhusu hali ya hewa, misimu na mazingira kutoka taarifa iliyo changiwa kupitia familia yake na jumuiya.
“Uelewa wa kina wa mifumo ya hali ya hewa, misimu na mazingira ni muhimu kwa uhai wa kila mtu. Kwa watu wa mataifa ya kwanza, miunganisho yetu ya kina kwa ujuzi huu, ilituwezesha kustawi katika hali hii tete ya mazingira.”,” Shangazji Joanne ame elezea.
Moodjar, the native Christmas tree Credit: TerriAnneAllen/Pixabay
“Kuna matukio mengi ya mazingira ambayo huathiri bara letu tete, iwapo ni dhoruba au ukame, watu wa Mataifa ya Kwanza wame watayarisha na wana ujuzi wa mifumo inayo ruhusu uponyaji kupitia vimbunga au kuelewa usalama katika dhoruba, nakufanya maandalizi ya ukame. Tunapo tazama jinsi hali hiyo ya hewa inavyo athiri watu wote, mara nyingi huwa tunataka kuwa na udhibiti, maarifa yetu ndiyo yanayo fanya tuwe salama. Diarra-murrahmah-coing, jua lina tua likiwa jekundu, hiyo ina maana hali ya hewa itakuwa nzuri kesho,” Shangaji Joanne amesema.
“Tunapotazama jinsi hali ya hewa inaweza waathiri binadamu wote, mara nyingi huwa tunataka kuwa na udhibiti, maarifa yetu ndiyo huhakikisha usalama wetu. Diarra-murrahmah-coing, jua linatua likiwa jekundu na, hiyo inamaana kwamba hali ya hewa itakuwa nzuri kesho.”
Katika upande wa magharibi ya Australia, msomi wa ujuzi wa maswala yaki asili katika chuo cha Murdoch Jordan Ah Chee, alizaliwa katika kanda ya Kimberley na ana mahusiano na watu wa ukoo wa Bindjareb, Wardandi, Palyku, Nyikina, na Yawuru.
“Kuna dhana hii kuwa watu wetu ni wahamaji ila, dhana hiyo ina egamia hoja kuwa hatuna mahali au hatuna kwetu."
We very much move with the seasons and we would move from place to place in a sustainable way.Jordan Ah Chee
“Wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait wamekuza uhusiano wa kina katika milenia, na ardhi, maji, anga na kupitia uhusiano huu tume unda maarifa haya ya kina ambayo yame tusaidia kustawi hapa na ni dhani hio kuwa kila kitu kina uhusiano.”
Uhusiano wa kina wa watu wa mataifa ya kwanza na ardhi, anga na maji, inaleta uelewa wa kina kwa jinsi mabadiliko ya misimu hu mulikwa katika mandhari.
“Kwa hiyo tofauti na namna za ujuzi wa magharibi ambako, una unganisha misimu kwa tarehe fulani kwenye kalenda, ujuzi wa wakati misimu inakuja na jinsi inavyo fuatana mwaka mzima, ulikuja kupitia mabadiliko kwa mandhari na mabadiliko kwa tabia za wanyama na mabadiliko kwa mazingira,” Ah Chee amesema.
“Na hiyo inge shawishi tuta kako kuwa wakati fulani wa mwaka, aina ya chakula kitakacho patikana, kama tutakuwa katika pwani au bara. Kwa hiyo uelewa wa hali ya hewa na misimu ilikuwa muhimu kwa hali yetu ya maisha.”
Fire stick farming Credit: Christian Bass/Unsplash
“Tunapo fikiria hili, pengine kitu cha kwanza ambacho huja katika fikra ni ukulima wa kijiti cha moto. ukulima wa kijiti cha moto hutu ruhusu kudumisha mafuta ndani ya ardhi ili kama moto una anza kwa sababu ya radi au matukio mengine, mafuta hayo hayatakuwa mengi sana,” Shangazji Joanne ame elezea.
“Ila, ina turuhusu pia kuhakikisha kuwa shina za kijani ziko tayari kwa aina za wanyama wanao zipenda.”
Mzunguko huo wakimsimu ume elezewa na watu wa mataifa ya kwanza, hutofautiana kulingana na sehemu waliko nchini Australia.
Katika nchi ya Noongar inayo patikana katika maeneo ya kusini-magharibi ya jimbo la Magharibi Australia, misimu sita hutambuliwa katika kalenda ya mwaka. Birak huashiria mwanzo wa msimu wa majira ya joto kuanzia mapema Disemba, wakati wa joto na sherehe.
“Birak “Birak ina husiana na joto, jua na moto. Ni wakati joto huongezeka na kawaida hujulikana kama msimu wa vijana na, ni wakati wa sherehe na msimu huu huashiriwa kwa nyoka na wanyama waki toa ngozi zao, vifaranga viki ondoka katika viota vyao na wanyama wachanga waki geuka kuwa wakubwa nakuanza maisha yao.,” Ah Chee ame elezea.
“Na badiliko lingine muhimu katika mandhari ni maua haya mazuri ya njano na rangi ya chungwa ya moodjar, au mti wa krismasi, ambao ni mti mhimu sana wakiroho wa watu wa ukoo wa Noongar. Na katika wakati huu, kutegemea na hali ya hewa na mazingira, ndipo kuchoma kwa kitamaduni kungefanyika”
Vitu vya mbinguni kama mwezi na mzunguko wayo, hutumiwa na watu wa Mataifa ya Kwanza kutambua mabadiliko ya hali ya hewa yanayo kuja.
In First Nation's knowledge systems moon halos depict the onset of rain.Aunty Joanne Selfe
“Katika mifumo ya maarifa ya mataifa ya kwanza, kivuli cha mwezi huashiria ujio wa mvua, ukifikiria hali hiyo chembe za barafu hu hifadhiwa angani, mwezi humulika na kumulika chembe hizo za barafu na inaweza sababisha muonekano wa kivuli kinacho zunguka mwezi. Sas ahata sayansi yakisasa inatambua kuwa vivuli vya mwezi mara nyingi hutangulia wakati wa baridi, mara nyingi ikifuatwa na mvua na nyuzi joto za baridi au, ndani ya siku ijayo au mbili”
Na mabadiliko ya hila kwa nafasi ya mwezi, pia yanaweza kuwa na maana muhimu.
“Ila wakati mwingine mwezi huwa hauko katikati ya kivuli hivho, unaweza kuwa upande mmoja kidogo na hiyo inaweza dokeza kuwa kuna upepe unao kuja pia,” Shangazi Joanne amesema.
A moon halo Credit: Geoffrey Wyatt
“Tuna baadhi ya sanaa aina ya petroglyphs mjini Sydney, chache sana kusema ukweli ila, moja ambayo ni nzuri sana ina itwa Moon Rock, ina michongo ya mwezi. Michongo hii inaonesha hatua nane za mwezi na zina anzia kwa boomerang ya muumba Biaime,” Shangazji Joanne amechangia.
“Hii ni muhimu kwa sababu wa Gaddy wanajulikana kama wavuvi wazuri sana, wanawake wetu daima walikuwa Warrang, bandari ya Sydney, wakivua Samaki na moto mdogo na mara nyingi walikuwa waki enda hapo na wato. Kwa hiyo tunapo tumia mwezi kuvua samaki, tunajua kuwa robo ya kwanza naya mwisho ya mwezi pengine ni wakati mzuri zaidi wakufanya uvuvi, na sababu yake ni kwamba mwezi mzima uta chochea mawimbi, yatakuwa na kasi zaidi na yatafanya iwe vigumu kuona samaki.”
Mazingira ya Australia yana utofauti mkubwa, unao zunguka dhoruba yaki tropiki, joto la jangwa na baridi ya alpine. Kila kanda ina midundo yake yakipekee.
Tumegundua jinsi, kwa jumuiya zawatu wa asili, misimu huwa hai elezewi kwa tarehe ila kwa jinsi mimea na wanyama hujibu mazingira yao. Mtazamo huu unatoa uelewa tajiri zaidi nawa kina wa mazingira ya Australia, kuliko mfumo wa kawaida a misimu mine.
Ni kumbusho imara la jinsi tamaduni zawatu wa asili zina uhusiano wa kina na ardhi na jinsi tunaweza jifunza kwa kutambua maarifa na tamaduni zao.
Kwa taarifa ya ziada kuhusu maarifa ya hali ya hewa yawa Australia wa Kwanza tembelea:
Subscribe or follow the Australia Explained podcast for more valuable information and tips about settling into your new life in Australia.