Ni nchi ambako maswala ya enzi za zamani naya kisasa hukutana, watu wengi wanao ishi vijijini wana endeleza imani zama babu wao, wakati mjini kuna kasi ya maendeleo yakiuchumi. Ila kutoka mgongano huu wa tamaduni, swala lakutisha lina endelea kukuwa na, watoto wa Uganda wana lipa gharama.
Watoto wanapotea na wanakuwa waathiriwa wa kafara ya binadam, kwa mikono ya 'washirikina' au wachawi. Imekadiriwa kuwa angalau watoto wawili hupotea kila wiki, mara nyingi watoto hao hutekwa kwa kafara zakiibada.
Wanaharakati wamesema, ongezeko la visa hivyo, ina husiana na umasikini, sera duni kuwahusu wachawi na takriban asilimia 80 ya umma inayo tafuta ushauri kutoka kwa waganga wakienyeji.
Onyo kwa wasilikilizaji, makala haya yana kera sana.