Chama cha Greens kime tangaza kita unga mkono muswada wakuanzisha mpango huo, pamoja na muswada wakujenga kwa ajili yakupanga. Chini ya mpango wa usawa wa pamoja, watu 40,000 wata weza nunua nyumba yao kwa ushirikiano na serikali kwa kutoa amana ndogo zaidi.
Seneta wa chama cha Nationals Matt Canavan amesema pendekezo la serikali ya shirikisho la marufuku ya matumizi ya mtandao kwa watoto wenye chini ya miaka 16 haistahili harakishwa ndani ya bunge. Muswada huo unatarajiwa kupigiwa kura ndani ya seneti kabla bunge limalize vikao vyake usiku wa Alhamisi. Matt Canavan amesema anataka marekebisho ya muswada, yanayo jumuisha kufutwa kwa data yakuthibitisha umri inapo tumiwa.
Chama cha Nationals cha Victoria kina kiongozi mpya. Mbunge Danny O'Brien wa Gippsland Kusini, ameteuliwa kuongoza chama hicho, na amechukua nafasi ya Peter Walsh ambaye amekuwa katika wadhifa huo kwa miaka 10.
Onyo la joto kali limetolewa kwa maeneo ya masharitki ya New South Wales hadi Alhamisi. Kesho imetabiriwa kuwa siku yeny ejoto zaidi katika maeneo ya Magharibi Sydney, ambako nyuzi joto zinaweza fika 40 na nyuzi joto 33 katika maeneo ya pwani. Nyuzi joto za juu zimetabiriwa kudumu hadi Alhamisi.
Mamlaka nchini Misri zimewaokoa watu 16 baada ya boti ya kitalii kuzama katika pwani ya Bahari ya Sham. Vyanzo vitatu vya usalama vimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa oparesheni za uokoaji zinaendelea kutafuta manusura zaidi. Kwa mujibu wa utawala katika eneo hilo, boti hiyo ilikuwa imebeba watu 45, wakiwemo watalii 31 na wafanyikazi 14.
Msemaji wa serikali ya Uganda amethibitisha kwamba kenya ilifahamu kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye. Matamshi yake yakija ikiwa imepita siku mbili baada ya Nairoibi kueleza kwamba ilikuwa imeanzisha uchunguzi katika tukio la kukamatwa kwa kiongozi huyo jijini Nairobi. Uganda imekashifiwa kwa kumteka Kizza Besigye wakati akihudhuria halfa ya uzinduzi wa kitabu cha mwanasiasa wa upinzani jijini Nairobi. Kulingana na msemaji wa serikali ya Uganda Chris Baryomunsi, Kampala na Nairobi zilifahamu kuhusu kukamatwa na kusafirishwa kwa Besigye.
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe ameachiwa kwa dhamana baada yake kuzuiliwa siku chache kuelekea uchaguzi wa mikoa. Chama kikuu cha upinzani katika taifa hilo la Afrika Mashariki, Chadema siku ya Ijumaa kilitibitisha kuwa Mbowe na viongozi wengine wa chama walikuwa wamezuiliwa kwa nguvu na maofisa wa polisi. Kwa mujibu wa chama, viongozi hao walikamatwa baada ya polisi kutawanya mkutano wao wa hadhara kwa mabomu ya machozi kusini mwa taifa hilo.