Taarifa ya Habari 19 Novemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Ripoti kuhusu mshikamano wakijamii imepata, kuna mitazamo michache chanya, kwa dini kote jimboni katika makundi yote makubwa ya imani.


Shirika la Scanlon Foundation limetoa ripoti yake mpya kuhusu mshikamano wakijamii, ripoti hiyo imeonesha viwango vya mshikamano vilivyo thabiti, wasiwasi kuhusu uchumi ukioneshwa kuwa moja ya vizuizi vikubwa.

Viongozi wa Kusini Australia wana piga jeki kampeni, yakuwa mwenyeji wa kongamano la mazingira la Umoja wa Mataifa. Kiongozi wa jimbo hilo Peter Malinauskas ana enda Azerbaijan wiki hii, kuhudhuria mkutano wa COP-29, ambako ata wasilisha kesi ya Adelaide kuwa mwenyeji wa kongamano la 2026. Australi ikichaguliwa kuwa mwenyeji wa kongamano la COP-31, itakuwa moja ya tukio muhimu laki diplomasia katika historia ya taifa hili.

Wanaharakati wanaomba uwekezaji zaidi kuhakikisha wazee nchini Australia wanao pitia uzoefu wa unyanyasaji, wanaweza pata huduma za misaada kote nchini Australia. Hatua hiyo inafuata kuwasilishwa kwa kampeni yakutoa uelewa ya serikali mnamo mwezi Julai, yenye thamani ya dola milioni $4.8 iliyo tolewa na serikali, ambayo ilikuwa na lengo laku chochea mjadala ndani ya jamii. Ina aminiwa mzee mmoja kati yawazee sita nchini Australia, unaweza pitia uzoefu wa unyanyasaji katika maisha yake, iwapo ni yakimwili, kisaikolojia, kihisia, kifedha au kingono.

Upinzani wa Mseto umethibitisha utapinda mpango wa serikali ya shirikisho kuweka vikomo kwa idadi ya wanafunzi wakimataifa wanao kuja kusomea nchini. Muswada wa serikali ya Labor wenye utata, utaruhusu idadi ndogo ya wanafunzi wakimataifa wa anze masomo yao nchini Australia mwakani. Idadi ya wanafunzi 270,000 ndiwo wata ruhusiiwa kuingia nchini. Kuna uwezekano muswada huo hauta pita bungeni bila msaada wa upizani wa mseto.

Serikali ya Tanzania imesema juhudi za uokozi zitaendelea hadi waathiriwa wote ambao wamekwama kwenye jengo la orofa nne lililoporomoka eneo la Kariakoo wameokolewa.
Idadi kamili ya wale wamenaswa ndani ya vifusi vya jengo hilo bado haijulikani. Watu kadhaa wameviambia vyombo vya habari nchini humo kwamba jamaa zao wanaoaminika walikuwamo ndani ya jengo hilo wakati wa mkasa, bado hawajulikani waliko. Tangu mkasa huo kutokea Jumamosi asubuhi, zaidi ya watu 80 wameokolewa, na idadi ya waliokufa imefika 13.

Urusi siku ya Jumatatu imezuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na ulinzi wa raia nchini Sudani baada ya kupiga kura yake ya turufu iliyopingwa na mataifa kadhaa wanachama ambao walitarajia kuweka shinikizo kwa majenerali wawili hasimu. Rasimu ya azimio ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi, inatoa wito kwa pande zote "kusitisha uhasama mara moja na kushiriki kwa nia njema katika mazungumzo ili kuwezesha hatua za kupunguza mgogoro, kwa lengo la kukubaliana kwa haraka juu ya usitishaji vita katika ngazi ya taifa. Rasimu hii iliyotayarishwa na Uingereza na Sierra Leone imepata kura 14 za ndio na moja inayopinga.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Dayosisi wa Nairobi Philip Anyolo ameagiza Rais William Ruto arudishiwe karibu Sh6 milioni ambazo alichanga kwa Kanisa Katoliki la Soweto, eneobunge la Embakasi Mashariki mnamo Jumapili. Pia ameamrisha Sh200,00o ambazo zilitolewa na Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja zirejeshwe akisema kuwa Mswada wa Mchango kwa Umma 2024 unasisitiza kuwa lazima kuwe na idhini kwa asasi ya umma inayolenga kuandaa au kunufaika kupitia mchango unaoshirikisha umma. Kiongozi huyo wa dini pia alisema kuwa ni kinyume cha kanuni za kanisa hilo kupokea pesa kutoka kwa wanasiasa akisema wanajihadhari na hali ambapo nyumba ya Mungu hutumika na wanaisa vibaya kucheza siasa.

Share