Upinzani watishia maandamano iwapo wanachama wao hawata achiwa huru Tanzania

Deputy Secretary General of Chadema Mr Salum Mwalimu

Deputy Secretary General of Chadema Mr Salum Mwalimu

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimetishia kuanzisha maandamano makubwa zaidi, tangazo linalokuja baada ya kutuhumu mamlaka kwenye taifa la Afrika Mashariki kwa kuwauua na kuwateka wanachama wake.


Chama cha Chadema Jumatano kimetishia kuandaa maandamano hayo katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam tarehe 23 ya mwezi Septemba. Chadema kinasema iwapo serikali haitochukua hatua ya kuchunguza na kueleza walipo wanachama wake waliotoweka basi hakitakuwa na buda bali kuitisha maandamano.

Kulikwepo na matumaini kwamba Tanzania ilikuwa inaingia katika kipindi kipya ya demokrasia chini ya utawala wake rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alichukua madaraka kutoka kwa mtangulizi wake John Magufuli aliyefariki mwaka mwezi Machi mwaka wa 2021.

Rais Samia ametangaza kupunguza baadhi ya marsharti ambayo upinzani na vyombo vya habari vilikuwa vimeekewa chini ya uongozi wa rais Pombe. Licha ya hayo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yameelezea wasiwasi wake kutokana na oparesheni za hivi karibuni ikiwemo kukamatwa na kuzuiliwa kwa wanachama wa upinzani walipokuwa katika mkutano wa kisiasa mwezi uliopita.

Share