Taarifa ya Habari 9 Agosti 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kiongozi wa upinzani Peter Dutton amesema chama chake kina endelea ku unga mkono makubaliano ya AUKUS, yaliyo tiwa saini chini ya serikali ya Morrison ila, ana hoji kwa nini serikali ya Albanese ina pinga nishati ya nyuklia.


Serikali ya shirikisho ime alikwa kuzungumza kuhusu uhaba mkubwa wama GP kote nchini. Ripoti ya Idara ya Afya na Huduma ya Wazee imesema kuwa, wakati kume kuwa ongezeko kwa idadi yama daktari, idadi hiyo bado haitoshi kushughulikia mahitaji ya huduma ya afya yawa Australia. Ripoti iliyopewa jina la 'Utoaji na mahitaji' ime onesha upungufu kitaifa wa zaidi yama GP 600 katika mwaka wa 2024, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi 1,900 katika mwaka wa 2028 na zaidi ya elfu 6 katika mwaka wa 2048.

Kamishna wa Watoto wa Australia ameomba pawe mtazamo wakitaifa kwa ulinzi wa watoto, akisema mifumo kote nchini ime lemewa. Katika jimbo la New South Wales, inagharimu takriban dola milioni moja kila mwaka, kutoa makazi kwa vijana ambao wako katika makazi ya dharura. Sasa ripoti mpya imeonesha kuwa mipangilio hiyo ya kuishi, inasababisha kukosekana kwa utulivu, kutengwa na ukosefu wa usimamizi.

Mataifa ya Kenya, Djibouti, Madagascar na Mauritius yamewasilisha rasimi majina ya watu wanaopendekezwa kuwania uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC. Nchi wanachama 55 kutoka mataifa wanachama wa AU zinatarajiwa kukutana katika kongamano la mwezi Februari mwaka ujao kumchagua mrithi wa mwenyekiti wa sasa Moussa Faki Mahamat. Mwaka huu, nchi wanachama wa EAC zimepwa nafasi ya kutoa mrithi wa Faki, raia wa Chad ambaye amehudumu tangu mwaka wa 2017. Umoja wa Afrika umechapisha majina ya watu wanne wanaowania nafasi hiyo akiwemo Mahamoud Ali Youssouf kutoka Djibouti, Raila Odinga wa Kenya, Richard Randriamandrato wa Madagascar na Anil Gayan raia wa Mauritius.

Mataifa ya Kenya, Djibouti, Madagascar na Mauritius yamewasilisha rasimi majina ya watu wanaopendekezwa kuwania uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi hapo jana, amemshutumu mtangulizi wake, Joseph Kabila, kwa kuchochea mzozo wa usalama mashariki mwa DRC kupitia Muungano wa (AFC). Katika mahojiano na Radio Top Congo, akiwa Brussels (Ubelgiji) ambako amekaa kwa siku chache kwa sababu za matibabu, Tshisekedi amesema alijaribu kuwasogelea wapinzani wake, lakini hawataki. Aidha ameeleza kwamba Moise Katumbi naye alikuwa na msimamo huo huo lakini kutokana na shinikizo kutoka upande wake, alikubali kuingia kwenye taasisi lakini anabaki nje.

Polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaomtaka rais ajiuzulu. Maandamano hayo ya Nairobi yaliandaliwa na wanaharakati waliokasirishwa na Rais William Ruto hata baada ya kuwatimua karibu mawaziri wake wote na kuwaongeza viongozi wa upinzani katika kile alichokiita serikali pana. Polisi pia waliweka vizuizi kwenye barabara za kuingia mjini.

Share