Chanzo cha mlipuko wa ugonjwa hatari wa legionnaires jimboni Victoria, kimetambuliwa mamlaka wa afya wakiamini ugonjwa huo umedhibitiwa. Mnara wakutoa baridi katika eneo la Kaskazini Laverton ambayo iko magharibi Melbourne imetambuliwa kama chanzo cha dazeni za kesi katika kitongoji hicho na kitongoji cha Derrimut wamepewa dawa. Clare Looker ni Afisa Mkuu wa Afya, amesema wana matumaini mlipuko huo sasa ume dhibitiwa. Hali hii inafutia mwanaume mwenye miaka 60 na mwanamke wa miaka 90, walio fariki baada yaku kabiliwa kwa mlipuko huo. Kuna kesi 77 zilizo thibitishwa kufikia leo, wote hao wame lazwa hospitalini.
Wasafiri jimboni Queensland watalipa tu senti 50 katika usafiri wa umma, wakati serikali ya jimbo ina jiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao. Punguzo hilo lita tumiwa katika translink bus, ferry na huduma za reli kwa miezi sita ijayo chini ya jaribio lenye lengo laku shughulikia shinikizo za gharama ya maisha. Bei za tikiti katika laini ya reli yakuenda uwanja wa ndege iliyo binafsishwa, imepunguzwa mara mbili chini ya mfumo huo.
Msemaji wa jeshi la Uganda amesema maafisa 100 wa polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbiliaUganda mwishoni mwa juma huku mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo yakipamba moto. Meja Kiconco Tabaro alisema siku wa Jumatatu (Agosti 5) kwamba maafisa hao wa polisi waliingia Uganda kupitia mpaka wa Ishasha katika wilaya ya Kanungu kusini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Tabaro alieleza kuwa polisi hao wa Kongo waliokuwa na bunduki 43 na risasi kadhaa walipokonywa silaha hizo.
Mwezi mmoja uliopita, kiongozi wa chama cha Labour nchini Uingereza Keir Starmer alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu. Chini ya wiki tano baadaye, serikali yake inapitia kipindi kigumu cha mgogoro: kwa siku sita, ghasia zilikuwa zimeongezeka nchini kote. Hali ii ilizuka kutokana na tukio la kuchomwa kisu wasichana watatu huko Southport mnamo Julai 29 na mlipuko wa habari ghushi mtandaoni, zinazotumiwa na mrengo wa kulia. "Ninahakikisha kuwa mtajuta kwa kushiriki katika machafuko haya," amesema Keir Starmer hivi pnde siku ya Jumapili jioni. Waziri Mkuu ameongoza mkutano wa dharura wa usalama leo Jumatatu asubuhi ili kukabiliana na machafuko hayo. Tangu mwanzo, chama cha Labour kimetumia maneno makali: hakuna suala la kuachia ngazi dhidi ya "majambazi wa mrengo wa kulia". Amewaahidi "nguvu kamili ya sheria". Lakini ghasia zinaendelea kuongezeka.
Maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali wamevamia ikulu ya Waziri Mkuu wa Bangladeshi siku ya Jumatatu mjini Dhaka, kulingana na picha za televisheni. Wakati huo huo Mkuu wa majeshi ametangaza kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na kuunda serikali ya mpito. ufuatia tangazo la kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, mkuu wa jeshi Waker-Uz-Zaman ameeleza kuwa majadiliano yanaendelea kuunda serikali ya mpito. Wawakilishi wa vyama vikuu vya siasa nchini wanashiriki katika majadiliano na jeshi, amesema.