Taarifa ya Habari 5 Novemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Wanaharakati wa Mataifa ya Kwanza wana muhamasisha Kiongozi wa Queensland David Crisafulli, abatilishe uamuzi wake wakufuta uchunguzi wakusema ukweli na uponyaji.


Chama cha Greens kina iomba serikali ya shirikisho ilete mbele mpango wayo waku punguza deni la wanafunzi kwa asilimia 20, kwa takriban idadi yawa Australia milioni 3, hatua ambayo itafuta zaidi ya $16 bilioni kutoka deni la wanafunzi.

Serikali ya Albanese ina panua mpango wa mafao wa hela taslim kama sehemu ya mkakati wa nguvu kazi katika idara ya ulinzi wenye thamani ya $600 milioni. Hii leo 5 Novemba serikali ya Albanese ilitangaza kuwa mpango wa nguvu kazi wa ulinzi wa 2024, kifurushi cha kuajiri na kuhifadhi chenye lengo laku zuia kuondoka katika jeshi la ulinzi la Australia. Mradi huo ulizinduliwa 2023, na jaribio hilo linatoa malipo ya $50,000 kwa wafanyakazi wakudumu wanao karibia mwisho wa huduma yao, waki ahidi kufanyakazi kwa miaka mitatu ya ziada.

Wamarekani wanajiandaa kupiga kura katika uchaguzi wa rais unaofanyika kesho Jumanne ambao utaamua mwanasiasa anayeiongoza dola hiyo yenye nguvu zaidi duniani katika kipindi cha miaka minne inayokuja. Makamu wa Rais wa sasa Kamala Harris kutoka chama cha Democratic anachuana na rais wa zamani Donald Trump wa Republican kuwania funguo za ikulu ya White House baada ya karibu mwaka mmoja wa kampeni. Zaidi ya Wamarekani milioni 77 tayari wamekwishapiga kura mapema na wagombea hao wawili wanatumai kuwahimiza mamilioni wengine kujitokeza kwa wingi kesho Novemba 5.

Rais mpya wa Botswana Duma Boko amechukua rasmi hatamu za uongozi wa taifa hilo leo Jumatatu, akimsifu mtangulizi wake kwa kufanikisha mabadilishano ya madaraka kwa njia ya amani. Boko amewaambia waandishi habari kwamba mabadilishano hayo ya madaraka ni uthibitisho wa kukomaa kwa demokrasia ya Botswana na mfano kwa maeneo mengine duniani.

Bunge la kitaifa limepokea ombi jipya linalopendekeza kupunguzwa kwa muda wa kuhudumu kwa viongozi waliochaguliwa kuwa mihula miwili pekee; sawa na ya rais na magavana. Ombi hilo, linalotarajiwa kuibua mjadala mkubwa nchini, limewasilishwa na kundi moja la kutetea haki za raia linaloendesha shughuli zake katika kaunti ya Nakuru.
Kulingana na kundi hilo, hatua hiyo inalenga kuweka usawa miongoni mwa wanasiasa na kutoa nafasi kwa wapiga kura kufaidi kutokana na talanta ambazo viongozi wengine wanazo.

Share