Taarifa ya Habari 4 Oktoba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Idara ya Afya ya New South Wales ina wahamasisha watu wanao stahiki wapate dozi zao mbili za chanjo za mpox sasa hivi, wasiwasi unapo endelea kuwa kuhusu ongezeko ya kesi na wanao lazwa hospitalini jimboni humo.


Australia imepata viti vya ziada 500 katika ndege ya abiria, katika jaribio laku ondoka Lebanon wakati uvamizi wa Israel unaendelea na milipuko yama bomu inasikika mjini Beirut. Wa Australia wenye asili ya Lebanon wamesema gharama ya hisia na kuvunjwa moyo kuhusu jamaa wao nchini Lebanon, inaongeza kwa uvamizi kamili wa nchi kavu wa Israel. Baadhi wamesema wana jamaa wao wazee wanao pokea huduma ya masaa 24 nchini Lebanon, ambao hawa wezi ondoka hatakama wanataka.

Vyama vidogo Jimboni Queensland vimesema vita unga mkono upinzani wa mseto wa Liberal National Party, katika uchaguzi wa jimbo ujao wa mwaka huu, vyama hivyo vime wahamasisha wapiga kura waweke chama cha Labor mwisho katika kura zao za upendeleo. Chama cha Bob Katter cha Australian Party kimesema kita unga mkono upinzani kwa mara ya kwanza, katika kanda ya Kaskazini Queensland, hatua ambayo inatarajiwa kushawishi matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 26.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatazamiwa kukutana na viongozi wenzake wa Kongo na Rwanda wiki hii kwa nia ya kuwashinikiza kuhitimisha "makubaliano ya haraka iwezekanavyo" kumaliza ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kulingana na chanzo katika Elysée. Rais wa Ufaransa atampokea kwanza rais wa DRC Félix Tshisekedi siku ya Ijumaa huko Elysée, kabla ya kukutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame siku ya Jumamosi kando ya mkutano wa 19 wa Francophonie, ambao utafanyika katika Grand Palais huko Paris. Emmanuel Macron "atahimiza pande hizo mbili kufikia makubaliano haraka iwezekanavyo ndani ya mfumo wa mchakato wa Luanda ili mapigano ya Kivu Kaskazini yafikie mwisho," kimesema chanzo hiki.

Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amekuwa akikabiliwa na tuhuma mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa nidhamu na kumhujumu mkuu wake Rais William Ruto. Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba Naibu Rais wa nchi hiyo Rigathi Gachagua siku ya leo amewasilisha ombi katika mahakama mjini Nairobi akitaka kusitishwa kwa mchakato wa kumuondoa katika nafasi yake ulioanzishwa dhidi yake na wabunge mapema wiki hii.
Washirika wa Rais wa Kenya William Ruto waliwasilisha maombi ya kuondolewa kwa Naibu rais Gachagua siku ya Jumanne wakimshtumu kwa kuchochea chuki za kikabila na kudhoofisha serikali. Gachagua anasema ametengwa na amekanusha shutuma za washirika wa Ruto kwamba alihusika na vurugu maandamano ya vijana maarufu Gen Z dhidi ya serikali mapema mwaka huu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesitisha kwa muda leseni ya maudhui ya mtandaoni ya gazeti la Mwananchi ikidaiwa kuchapisha maudhui yanayoleta tafsiri hasi kwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Hatua ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya kusimamisha kwa muda leseni ya kampuni ya habari ya Mwananchi Communications Ltd(MCL) imetafsiriwa tofauti na wadau wa Habari Tanzania, ambao wameikosoa kanuni ya maudhui mtandaonina kusema inaacha mwanya wa tafsiri tofauti.

Share