Taarifa ya habari 4 Novemba 2024

Bench - Swahili.jpg

Chama cha Greens kina omba serikali ya shirikisho ilete mipango yake mbele yaku kata deni la wanafunzi kwa asilimia 20 kwa idadi yawa Australia milioni tatu, hatua ambayo itafuta zaidi ya deni ya wanafunzi yenye thamani ya dola bilioni 16.


Waziri Mkuu Anthony Albanese alitangaza ahadi ya sera wikendi iliyopita kama sehemu ya kampeni kabla ya uchaguzi mkuu wa shirikisho ujao. Pendekezo hilo linaweza futa kwa wastan $5,520 kutoka madeni ya wanafunzi hao (ikifunika chuo kikuu, elimu ya ufundi, na mikopo ya msaada wa mafunzo) kuanzia 1 Julai 2025. Wanafunzi watakao kuwa namadeni kuanzia 2026 kuendelea, hawata faidi kupitia sera hiyo.

Uamuzi wa serikali mpya ya chama cha Liberal cha Queensland, kusitisha uchunguzi wa kusema ukweli na uponyaji wa waAustralia wa kwanza, umekosolewa na wahanga wa vizazi vilivyo ibiwa. Imekadiriwa kuwa mtoto mmoja kati ya watoto waki Aboriginal na Torres Strait, wali ondolewa kwa nguvu kutoka familia zao kati ya mwaka wa 1910 na 1970 chini ya sera za serikali. Kiongozi mpya wa jimbo hilo David Crisafulli, amesema vikao vijavyo katika visiwa vya Cherbourg na Stradbroke [[Minjerribah/Terrangerri]], hauta endelea akiongezea kuwa hataki uamuzi huo kusababisha mgawanyiko. Mwenyekiti wa bodi ya shirika la Healing Foundation, Profesa Steve Larkin, amesema uamuzi huo ni tendo laku gawanya lenyewe na itaongeza kwa maumivu na mateso ya wahanga wa vizazi vilivyo ibiwa.

Watu 14 waliuwawa kwa kupigwa na radi kwenye  kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda, polisi walisema leo Jumapili. Watu 14 waliuwawa kwa kupigwa na radi kwenye kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda, polisi walisema leo Jumapili. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi katika wilaya ya Lamwo. Msemaji wa polisi Kituuma Rusoke alisema watu wengine 34 walijeruhiwa. Waathirika bado hawajatambuliwa, aliongeza. Radi mbaya kwa kawaida huripotiwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki wakati wa misimu ya mvua. Rusoke alisema hakuna taarifa ya moto kuzuka kufuatia radi hiyo.

Takriban watu 13 wameuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumapili katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo la RSF katika jimbo la Al-Jazira kusini mwa Khartoum nchini Sudan. Chanzo kimoja kilichozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, kimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kikosi cha RSF, kiliwafyatulia risasi watu hao waliokuwa katika mji wa Al-Hilaliya. Jimbo la Al-Jazira nchini imekuwa eneo kuu la mapigano kufuatia kutoka kwenye kikosi hicho cha RSF kwa kamanda mmoja Abu Aqla Kaykal.

Mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris anafanya kampeni huko Michigan  Jumapili huku mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump akisimama katika majimbo matatu ya mashariki yenye ushindani Mkali Kura za maoni zinaonyesha ushindani mkali wa karibu sana kihistoria na ukusanyaji maoni uliofanywa na New York Times na Siena uliochapishwa siku ya Jumapili umewaonyesha Makamu wa Rais Harris na Rais wa zamani Trump wakiwa sawa katika majimbo saba ambayo huenda yakaamua matokeo ya Jumanne.

Nahodha wa mchezo wa kriket wa Australia Pat Cummins, atarejea uwanjani dhidi ya Pakistan katika mechi ya kwanza yakimataifa ya siku moja ya majira ya joto dhidi ya Pakistan leo saa nane unusu 4 Aprili katika uwanja wa M-C-G. Mchezo huo wa mechi tatu ulianza katika uga wa MCG, timu zote mbili ziki jiandaa kushiriki katika mashindano yama bingwa. Cummins amesema anatarajia kurejea katika mechi yake ya kwanza tangu kombe la dunia la T20 mwezi Juni na, anatarajia mapambano makali. 

Rais wa shirikisho la Riadha ya Australia Jane Flemming amesema kuongezwa kwa Marathon ya Sydney, katika Marathon sita kubwa za dunia, ni wakati wa mabadiliko kwa riadha ya Australia. Ni mashindano ya kwanza tangu Tokyo 2013, itakayo kamilisha mbio za marathon za Boston, London, Berlin, Chicago na New York City.
Bi Flemming amesema anatarajia mafanikio hayo yata wapa moyo wa Australia wengi kuanza kushiriki katika riadha.

Share