Data ya hivi karibuni imeonesha kwa sasa ni ghali zaidi kununua nyumba Adelaide au Perth kuliko Melbourne. Kulingana na takwimu mpya za kampuni ya CoreLogic, faida katika miji yenye idadi ndogo ya watu iliongeza bei ya kitaifa kwa nusu asilimia mwezi uliopita. Faida ya kati ya nyumba ya Australia iliongezeka pia nakufika laki $800 (($802,357)) kwa mara ya kwanza.
Kampeni mpya ya afya inawahamasisha watu wazingatie asili zao kama njia yaku boresha vyakula vya mchana vinavyo andaliwa nyumbani. New South Wales Multicultural Health Week imesema mwelekeo tofauti kwa aina ya vyakula vinavyo tolewa kwa watoto, vinaweza saidia kuunda tabia za ulazi za maisha yote. Mandhari muhimu niku ongeza matuna na mbonga za majani ndani ya boxi za chakula cha mchana, kwa ajili yakutoa motisha kwa aina ya vyakula jamii tofauti hula nyumbani.
Waandamanaji mjini Tel Aviv waliendelea mpaka usiku Jumatatu kushinikiza makubaliano ya haraka kuhusu mateka katika maandamano makubwa ambayo yaliongezeka siku ya Jumapili, baada ya mateka sita wa Israel kukutwa wamekufa katika handaki huko Gaza.
Hayo yamejiri wakati chama kikuu cha wafanyakazi kikianza mgomo mkubwa wa saa 24 kuihimiza serikali kufikia makubaliano na waandamanaji, ambao awali walikuwa wakijaribu kuzuia mkutano wa Waziri mkuu Benjamin Netanyahu na vyombo vya Habari, wakichoma moto mbao huku wakibeba mabango na kucheza ngoma. Safari za ndege, huduma za usafiri na hospitali zimetatizwa kwa kiasi kikubwa wakati waandamanaji wakimtaka waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuwarudisha nyumbani mateka 101 waliobaki kutoka Gaza, jambo linalodhihirisha mgawanyiko mkubwa ndani ya Israel kuhusiana na mbinu yake.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefanya mazishi ya miili ya watu 200 waliofariki dunia katika mazingira ya aina mbalimbali kwenye makambi ya wakimbizi wa ndani karibu na mji wa Goma. Maombolezo yalifanyika kwenye uwanja wa michezo mjini Goma ambapo viongozi mbalimbali kutoka serikali kuu walishiriki. Watu hao ni wale waliofariki tangu kuzuka kwa vurugu baina ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 miaka minne iliyopita kwenye eneo hilo.
Wizara ya afya nchini Uganda imetangaza ugonjwa hatari wa Homa ya Nyani umesambaa katika kila sehemu ya taifa hilo la Afrika mashariki na kuwataka wananchi kutoa taarifa mapema wanapomuona mtu mwenye dalili hatarishi. Mamlaka za afya sasa zimo mbioni kudhibiti kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo ambapo hofu ni mashaka ni kwamba ni kipindi cha likizo ya shule na watoto wamerudi makwao wakisafiri kutoka sehemu moja ya nchi hadi nyingine. Tarehe 24 mwezi Julai mwaka huu, kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Homa ya Nyani kiliripotiwa kwenye mji wa Bwera wilaya ya Kasese mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.