Taarifa ya Habari 29 Oktoba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Faini kwa watoa huduma wa NDIS wasio waaaminifu zita ongezeka kutoka $400,000 hadi zaidi ya $15 milioni, chini ya kanuni mpya zilizo zinduliwa na Bill Shorten jana Jumatatu 28 Oktoba 2024.


Waziri wa mfumo wa bima yakitaifa ya ulemavu amesema, mageuzi yata saidia mdhibiti kuwaondoa waendeshaji wasio waaminifu. Tume ya ubora na ulinzi ya NDIS itapata pia mamlaka mapya ya kuzuia na kuwasilisha mashtaka.

Kundi la nishati safi lime kosoa pendekezo la nyuklia la upinzani wa mseto, katika kikao cha bunge kwa uwezekano wa matumizi ya nishati hiyo mjini Canberra. Baraza ya Nishati Safi imesema ina amini mpango huo hau husu kusaidia kupunguza bili za nishati zawa Australia nakuwa nia halisi ya upinzani wa mseto niku shambulia ukuaji wa sekta ya nishati mbadala.

Walimu jimboni New South Wales wamefikia makubaliano mapya ya malipo ya miaka mitatu, baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo na maafisa wa serikali. Mkataba ulio tiwa saini na chama cha shirikisho cha walimu wa NSW, unajumuisha nyongeza ya malipo ya kima cha chini ya asilimia tatu kwa miaka mitatu ijayo pamoja na mazingira bora yakufanyia kazi.

Muungano wa Common Front for Congo (FCC) wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa DRC kinapinga dhidi ya rasimu ya marekebisho ya Katiba iliyowasilishwa na Rais Félix Tshisekedi wiki iliyopita. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni ya Jumapili Oktoba 27, muungano wa rais wa zamani umetoa wito wa "kuzuia" mageuzi kupitia "uhamasishaji". Kambi ya Joseph Kabila pia ilitaka kufanyia marekebisho katiba mwaka 2015, na kuamua kusitisha mradi huo baada ya kupingwa na maandamlano raia na Kanisa. Wiki iliyopita, akiwa Kisangani, Rais Félix Tshisekedi alithibitisha nia yake ya mageuzi hayo na akataja kuanzishwa mwaka 2025 kwa tume maalum ya wataalam.

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi, Patricia Kaliati alifikishwa katika mahakama ya Lilongwe leo Jumatatu, ambapo alishtakiwa rasmi kwa kupanga njama za kumuua rais Lazarus Chakwera. Polisi nchini Malawi walimkamata Kaliati, katibu mkuu wa chama cha upinzani cha United Transformation Movement (UTM), Alhamisi iliyopita kwa kupanga uhalifu. Kaliati, mbunge tangu mwaka 1999 ambaye ameshikilia nyadhifa kadhaa za uwaziri anaongoza UTM ya makamu wa rais wa zamani Saulos Chilima, aliyefariki katika ajali ya ndege mwezi Juni. Kufuatia kifo chake, chama hicho kilijitoa katika muungano wa vyama tawala ambao uliungana ili kuwezesha muungano wa Chakwera kushinda uchaguzi wa 2020.

Idadi ya vijana wanaoumwa saratani nchini Kenya inazidi kuongezeka. Takwimu zinaonyesha karibu vijana laki moja, wanaugua ugonjwa huo. Wahudumu wa afya wamelihusisha ongezeko hili na kutozingatia lishe bora. Wahudumu wa afya wanasema kuna umuhimu mkubwa wa kuendesha uhamasishaji miongoni mwa vijana ikizingatiwa kundi hili la raia mara nyingi hawaamini kwamba wanaweza wakapata saratani, ugonjwa huu ukiwa ungali unahusishwa na watu walio na umri mkubwa. Kulingana na muungano wa mashirika ya saratani nchini Kenya, takwimu za sasa za maradhi ya saratani miongoni mwa vijana ni virusi vya HPV vinavyosambazwa kwa ngono vikihusishwa na ongezeko hili wito ukitolewa kwa vijana kuwa makini katika mahusiano yao ya kimwili.

Share