Taarifa ya Habari 28 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Vyama vya wafanyakazi wanaunga mkono haki ya wabunge wa chama cha Labor kuvuka sakafu na kupiga kura dhidi ya msimamo wa chama, wakisema hatua hiyo ina imarisha vuguvugu la Labor.


Hali hiyo imejiri baada ya Seneta Fatima Payman kujiunga na wanachama wa Greens wiki hii, kupiga kura yakutambua Palestine kuwa taifa. Viongozi wa ngazi za juu wa chama cha Labor waziri wa maswala yakigeni Penny Wong akijumuishwa, wamesema uamuzi wa waziri mkuu Anthony Albanese wakutomfukuza au kumsimamisha kazi, ulionesha kiwango kikuu cha kujizuia. Waziri Mkuu alimzuia Seneta Payman kuhudhuria mkutano mmoja tu wachama wiki ijayo, kabla bunge liende katika mapumziko ya majira ya baridi.

Watetezi wameomba pawe huduma zaidi zinazo zingatia utamaduni baada ya ripoti kupata kuwa wanawake walikuwa wakipitia visa vya unyanyasaji wa nyumbani katika umma kwa ujumla ila, hawakuwa wakiripoti visa hivyo. Ripoti kutoka chuo cha Wollongong na shirika la Settlement Services international, ya kwanza yakipekee, ilifanya utafiti katika wanawake wakimbizi 300 wenye miaka kati ya 18-30 nakupata karibu 1 kati ya 3 wamepitia uzoefu wa unyanyasaji wa nyumbani. Wanawake katika ripoti hiyo walisema kuzungumza na mfanyakazi wa kike na mtu katika lugha yao, yalikuwa baadhi ya maswala muhimu, kuwezesha majadiliano kuhusu unyanyasaji wa nyumbani.

Kampuni ya Meta imesema chaguzi zote ziko mezani kuhusiana na kama kampuni hiyo, ita ondoa taarifa za habari kutoka mitandao yake nchini Australia iwapo hatua hiyo itawekwa chini ya kanuni za majadiliano ya vyombo vya habari yakulipia taarifa ya habar.
Wakati wa kikao cha bunge kuhusu mitandao ya habari, Mkurugenzi wa Kanda wa Australia Mia Garlick, amekiri kuwa hatakama serikali haija tangaza mipango yake, kufuata kunge onekana tofauti kama sheria zingetumiwa kwa Meta. Amesema kile ambacho watu wanafanya katika mitandao kama Instagram na Facebook, kime badilika katika miaka iliyo pita, 50% ya muda wao kwenye Instagram sasa hutumiwa kwa video zinazo chapishwa katika mtandao huo. wa watu wengi wanao tumia Facebook, chini ya asilimia 3 ya vyanzo vyao vya taarifa ya habari imepungua kwa asilimia 80 katika matumizi ya taarifa ya habari kwenye Facebook.

Polisi nchini Kenya wameweka vizuizi vya barabarani kwenye mitaa inayoelekea kwenye makaazi ya rais siku ya Alhamisi. Hayo yanafanyika wakati waandamanaji wakisisitiza kuyavamia na kuyakalia makaazi hayo, licha ya Rais William Ruto kutangaza kuuondosha muswada wa fedha unaozozaniwa wa mwaka 2024, uliochochea maandamano makubwa.
Haikuwa wazi ni kwa umbali gani waandamanaji hao wangeridhishwa na uamuzi huo wa Rais Ruto, Jumatano siku moja baada ya machafuko yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 23 na kushuhudia bunge likivamiwa. umeshuhudiwa maandamano na mahali pengine utulivu siku ya Alhamisi nchini humo na hakukuwa na purukushani kama zilizoshuhudiwa huko nyuma. Ruto anakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi katika kipindi cha utawala wake wa miaka miwili, wakati wasiwasi ukizidi kufuatia maandamano yanayoongozwa na vijana kutokana na shutuma za ongezeko la kodi.

Shirika la kimataifa la fedha (IMF) Jumatano limesema bodi yake ya utendaji imekamilisha tathmini ya tatu ya mpango wa kuirahisishia Zambia kuendelea kupata mikopo na imeidhinisha mkopo wa mara moja wa dola milioni 569.6. Bodi hiyo imeidhinisha pia ombi la Zambia la kuiongezea msaada wa kifedha kutoka dola bilioni 1.3 hadi dola bilioni 1.7 ili kulisaidia taifa hilo la Kusini mwa Afrika kukabiliana na ukame mbaya, ambao ulisababisha hasara upande wa mazao na kuathiri uzalishaji wa umeme. Katika taarifa, afisa wa IMF Antoinette Sayeh amesema mamlaka za Zambia zilipiga hatua ya kuridhisha kuhusu mageuzi ya kiuchumi na kimkakati, huku zikikabiliana na changamoto za kibinadamu kutokana na ukame.

Wanajeshi wawili wa Afrika Kusini wameuawa wakati wengine 20 wakijeruhiwa katika shambulio la roketi mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jeshi limethibitisha. Wanajeshi wa Afrika Kusini wametumwa nchini DRC kama sehemu ya vikosi vya nchi za SADC kujaribu kusaidia kurejesha usalama katika eneo la mashariki ya nchi pamoja na kudhibiti uasi zaidi. Kwa mujibu wa jeshi la Afrika Kusini, moja ya kambi zake mashariki ya DR Congo ilishambuliwa siku ya Jumanne. Shambulio hilo limethibitishwa kutokea katika mji wa Sake, Kilomita 25 sawa na maili 14 Magharibi mwa mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Share