Mwanzilishi huyo wa shirika la Wikileaks aliwasili nchini Australia masaa machache baada yaku kubali kuwa na hatia ya kosa moja la ujasusi katika mahakama moja ya marekani. Waziri Mkuu Anthony Albanese alichapisha picha yake kwenye mtandao wa X akimpigia simu Julian Assange, alisema "alifurahia kuzungumza na Julian Assange kumkaribisha nyumbani kwa familia yake nchini Australia." Hata hivyo, Seneta Birmingham amesema hatua hiyo haiku faa.
Ongezeko kwa mfumuko wa bei ya asilimia 4, imeweka serikali katika hali ya ulinzi inapo jaribu kutafuta namna yaku hakikishia familia zawa Australia kuwa chama cha Labor kina elewa maumivu yao. Hatua inayo fuata kwa viwango vya riba iko mashakani wakati benki ya hifadhi ya Australia ikipanga kutoa namba inayo kubalika. Muda wa kusubiri viwango vya riba unaweza kuwa mrefa wachumi sasa wakionya, kuna uwezekano wa ongezeko wa kiwango katika mkutano mwingine wa bodi mnamo Agosti. Ila Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema chama cha Labor kina sera zaku kabiliana na ongezeko la kiwango cha riba.
Utafiti mpya umepata kuwa theluthi tatu ya wanawake ambao wamekuja Australia katika miaka mitano iliyopita, wamepitia uzoefu wa aina fulani ya unyanyasaji kutoka kwa wachumba wao. Chuo cha Wollongong na shirika la Settlement Services International zime fanyia tathmini uchunguzi michakato ya unyanyasaji wa nyumbani uliolengwa kitamaduni katika mashirika Matano yanayo toa huduma ya makazi kwa wakimbizi. Utafiti huo ni wa kwanza nawa kipekee nchini Australia ambako, takriban wanawake 355 wenye miaka kati ya 18 hadi 80 kutoka nchi 24 walishiriki katika utafiti huo. Mradi huo ulipata kuwa uchunguzi katika shirika la settlement services, uliwasaidia wanawake kuzungumzia uzoefu wao nakupewa msaada.
Rais wa Kenya Dr. Willam Ruto ametupilia mbali mswada wa fedha wa 2024 uliozusha utata na maandamano makubwa nchini humo na kusababisha vifo na uharibifu wa mali. Akihutubia taifa kutoka Ikulu ya Nairobi, Ruto amesema anakubali kwamba wananchi wametoa kauli yao na amewasikia. Ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya serikali, Ruto ametangaza hatua mbali za kupunguza matumizi ya pesa ikiwemo kusitisha miradi mbalimbali ya maendeleo, kupunguza bajeti katika ofisi ya Rais, wizara mbalimbali, bajeti ya bunge na serikali za kaunti. Aidha ameeleza kwamba kwa kila shilingi mia moja ya kenya inayokusanywa, shilingi sitini na moja zinatumika kulipa madeni na kwa hivo itabidi wakenya kuishi kulingana na uwezo wao katika nchi hiyo yenya mzigo mkubwa wa madeni, ambapo asilimia 60 ya bajeti inatumika kulipa madeni.
Wataalamu wa haki za binaadamu wanaoufanyia kazi Umoja wa Mataifa wamezituhumu pande zinazozozana nchini Sudan kwa kutumia njaa kali kama silaha ya vita. Hayo ni wakati kukiwa na onyo linaloongezeka kuhusu kuzuka kwa baa la njaa nchini humo. Wataalamu hao wamesema vikosi vya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF vinatumia chakula kama silaha na kuwaacha raia wateseke kwa njaa. Wanasema kiwango cha njaa na watu kupoteza makaazi yao kinachoonekana nchini Sudan hakijawahi kushuhudiwa kabla. Mapigano yaliyodumu kwa miezi 14 yamewauwa zaidi ya watu 14,000 na kuwajeruhi wengine 33,000, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, lakini wanaharakati wa haki wanasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Katika michezo...
Umati mwingine mkubwa wa mashakibi unatarajiwa kwa mechi ya kwanza yaku amua mshindi wa michuano ya State of Origin wa wanawake. Queensland watakuwa na upendeleo mkubwa wa nyumbani watakapo kabiliana na Sky Blues wa NSW mjini Townsville katika mechi ya tatu ya michuano hiyo. Ni mara ya kwanza wanawake wame cheza mechi ya tatu kuamua mshindi, kabla walikuwa wakicheza mechi moja hadi mwaka wa 2023 ambako mechi bili zili ongezwa, kisha mechi ya tatu ikaongezwa baadae.
Maroons wa Queensland walishinda mechi ya mwisho kwa alama moja dhidi ya NSW.