Shirika la Anglicare Australia limesema mfumo wa ushuru unachangia kwa ukosefu wa usawa wa utajiri. Shirika hilo limetoa ripoti inayo tazama ugavi wa mali katika muda wa miongo miwili. Ripoti ya 'Ongezeko la Pengo' imefichua kuwa wa Australia matajiri wana kiwango cha mali mara tisini kulinganishwa na wale wenye hela chache zaidi.
Mweka hazina wa shirikisho Jim Chalmers ametumia hotuba kwa swala la mshikamano wakijamii, kumuita kiongozi wa upinzani 'kiongozi anayegawanya zaidi' wa chama kikubwa katika historia ya Australia. Mweka hazina alitoa madai hayo katika hotuba yake mbele ya wanachama wa Labor usiku wa jana Jumatatu 26 Agosti mjini Melbourne, miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025. Dr Chalmers amesema siasa ya Australia kwa sehemu kubwa haijawa na vurugu yakisiasa ila, hali hiyo haistahili puuzwa kwa upande wa uongozi unao epuka siasa zakugawanya. Alimshtumu Bw Dutton kwa kukumbatia mgawanyiko, akiongezea kuwa hali hiyo ni "hatari".
Watoto walio pona majaribio yakutolewa kafara na waganga wakienyeji katika taifa moja la Afrika, wanapokea matibabu yakubadilisha maisha yao bila malipo nchini Australia.
Waganga wakienyeji hudai kuwa viungo vya mwili na damu ya watoto vinaweza fanya miujiza, utajiri na afya kwa wateja wao. Kufikia sasa, watoto watano wame letwa Australia kupokea matibabu, gharama zao zote zimefunikwa zimeshughulikiwa na michango ya mashirika ya misaada kama Kyampisi Childcare Ministries. Ila kuna watoto wengi nchini Uganda ambao bado wanasubiri fursa yao.
Misri imesema haitakubalina na hatua ya vikosi vya Israel kuendelea kuwepo kwenye mpaka wake na Ukanda wa Gaza, vyombo vya habari vyenye uhusiano na serikali vimeripoti hii leo. Cairo, ambayo ni miongoni mwa wapatanishi wakuu katika juhudi za kupatikana kwa makubaliano kati ya Hamas na Israel kuelekea vita vya Gaza, imeziambia pande zote kwamba haitakubali uwepo wa aina yoyote wa jeshi la Israel katika ukanda wa kimkakati wa Philadelphi, shirika la habari la Al-Qahera lenye uhusiano na serikali limesema likinuu duru za ngazi za juu. Hoja ya msingi katika mazungumzo ya kusitisha mapigano imekuwa ni wito kwa Israel kuondoa vikosi vyake katika eneo hilo, pamoja na kivuko cha Rafah, ambacho ni pekee kutoka ardhi ya Palestina ambacho hakikudhibitiwa moja kwa moja na Israel.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga anatarajiwa kuaga rasmi siasa za Kenya, ambapo uwanizi wake wa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) utazinduliwa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi. Rais Ruto, baraza lake lote la mawaziri, maafisa wa ngazi za juu serikalini, kesho asubuhi watakongamana katika Ikulu ambapo azma ya Bw Odinga itazinduliwa na kuhudhuriwa na Marais kutoka nje ya nchi pia. Uchaguzi wa AUC utaandaliwa Februari 2025 na kiongozi huyo wa ODM anaonekana kama mwanasiasa ambaye yupo kifua mbele kuwahi kiti hicho. Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Salva Kiir Mayardit (Sudan Kusini), Samia Suluhu (Tanzania), Hassan Sheikh Mohamud (Somalia), Waziri Mkuu wa Burundi Gervais Ndirakobuca na Waziri wa Masuala ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe kufikia leo walikuwa wamethibitisha kuwa watakuwa katika hafla hiyo.
Dozi Elfu 10 za Mpox za kwanza zinatarajiwa kuwasili barani Afrika Kuanzia wiki hii, wakati huu pia maambukizo zaidi yakiendelea kuripotiwa hali iliyofanya shirika la afya duniani kutangaza ugonjwa huu kama janga la kidunia. Chanjo hizo zinaletwa Afrika baada ya mataifa zaidi ya 70 nje ya Afrika kuwa nazo, dhihirisho kuwa mafunzo kutokana na uviko 19 ambapo Afrika ilibaguliwa katika usambazaji wa chanjo ,bado hayajaweza kuleta mabadiliko. Kwa mujibu wa taasisi ya kudhibiti magonjwa barani ,Afrika CDC, ucheleweshaji huu ambao umelazimu Afrika kutegemea chanjo za msaada ni kuwa sababu kampuni za kuzalisha chanjo zilihitaji kupata idhini kutoka WHO ,idhini ambayo imetolewa mwezi huu.