Australia imepatwa inatoa uzalishaji mwingi usio wa uwiano kutoka kwa uchimbaji wa mafuta miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya zamadola, katika ripoti iliyo tolewa na Waziri Mkuu wa Tuvalu Feleti Teo. Australia imetia saini mkataba wakihistoria na Tuvalu, mkataba huo unawaruhusu raia 280 taifa hilo kuhamia Australia kila mwaka, taifa hilo la Pasifiki linapo endelea kukabiliana na ongezeko la janga la ongezeko ya viwango vya maji ya bahari.
Viongozi wa Queensland wana fanya kampeni za mwisho kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi wa jimbo utakao fanywa kesho jumamosi, kura za maoni mpya zinadokeza kuwa chama tawala cha Labor kinatarajiwa kushindwa baada ya takriban muongo mamlakani. Kiongozi wa jimbo hilo Steven Miles ame ahidi kutembelea maeneo bunge 36 katika siku za mwisho za kampeni, wakati imeripotiwa kiongozi wa upinzani David Crisafulli anategemea kushindi maeneo bunge yote tatu ya Townsville kwa ajili yakuwa na wingi bungeni, maeneo bunge hayo kwa sasa yako chini ya uongozi wa chama cha Bob Katters' Australian Party. Kura ya maoni ya Newspoll iliyo fanya na gazeti la The Australian imedokeza kuwa upinzani una ongoza serikali ya Labor, baada ya kura za upendeleo licha ya chama cha Labor na Steven Miles kuongeza ushawishi wayo katika wiki za hivi karibuni.
Marufuku iliyo subiriwa kwa muda mrefu kwa wamiliki wa nyumba kuwafurusha wapangaji bila sababu yoyote, imepitishwa na bunge la New South Wales. Rose Jackson ni waziri wa nyumba jimboni humo, ame elezea mabadiliko hayo kuwa ya moja kwa moja na ya busara, na hatua ambayo itarejesha usawa katika soko ghali zaidi la kodi nchini.
Ila wanaharakati wamesema mengi zaidi yanastahili fanywa.
Waziri wa fedha wa Australia ametangaza kuwa mfumuko wa bei wa ndani una endelea kuwa wastan, kabla ya kutolewa kwa takwimu za bei za wateja za kila robo wiki ijayo. Utabiri mpya kutoka Shirika la Fedha lakimataifa lina onesha Australia kama nchi inayo zembea katika vita vyakimataifa dhidi ya mfumuko, mataifa mengine mengi Marekani ikijumuishwa, zinapunguza tayari viwango vya riba. Serikali ya Labor imekuwa chini ya shinikizo kuthibitisha mkakati wayo wa uchumi una tumika, wakati uchaguzi mkuu wa shirikisho unakaribia na gharama kubwa ya maisha ina waumiza wapiga kura.
Rais William Ruto anazongwa na mizozo mingi ya kisheria na kisiasa inayoongezeka kila uchao kesi kuhusu kuondolewa kwa naibu wake Rigathi Gachagua zikiwa za hivi punde.
Hata baada ya kushinda kesi ya ushuru wa Nyumba Mahakama Kuu ilipoamua Jumanne kuwa sheria iliundwa kikatiba, mzozo huo unaonekana kuelekea katika mahakama ya Rufaa baada ya Dkt Magare Gikenyi na walalamishi wengine kuapa kupinga uamuzi huo.
Kwa siku tatu mfululizo ,waasi wa M23 pamoja na makundi ya vijana wazalendo wanaoungwa mkono na serikali ya Kongo, wanapigania udhibiti wa mji muhimu wa Kalembe wilayani Walikale. Mji huo uliotangazwa kukombolewa hapo Jumatatu na makundi ya vijana hao wazalendo baada ya siku moja kuchukuliwa na M23, sasa ni kitovu cha mapigano kati ya pande zote mbili. Kulingana na vyanzo vya ndani, leo Jumatano wapiganaji wa kundi la M23 wamezidisha mashambulizi yao katikati mwa mji huo.
Uganda imeripoti kifo cha kwanza kilichosababisha na ugonjwa wa Mpox. Hayo yametangazwa na Waziri wa afya wa nchi hiyo Jane Ruth Aceng ambaye amesema hatua lazima zichukuliwe kukabiliana na hali hiyo. Waziri wa afya wa nchi hiyo Jane Ruth Aceng amefahamisha kuwa kifo hicho ni kielelezo kinachoonesha, hatua madhubuti zinastahili kuchukuliwa katika kukabiliana na kasi ya maambukizi ambayo kwa sasa idadi ya watu 153 wamekutwa na virusi vya ugonjwa huo. Waziri huyo ameagiza majopo yaliyohusika katika kupambana na UVIKO-19 kwenye ngazi za wilaya kuitwa tena kushiriki kwenye juhudi za kupambana kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.