Sheria hizo mpya zina maana kuwa maafisa wa polisi wanaweza tumia vifaa vyaki elektroniki kufanya msako situ ndani ya usafiri wa umma na ndani ya maeneo salama ya burudani usiku ila pia ndani yama soko, katika sehemu za michezo na burudani na ndani ya vituo vya reli. Hatua hizo zita fanyiwa majaribio hadi 2026 ambapo zitafanyiwa tathmini kuhakikisha hazitumiwi vibaya.
Waziri wa Afya Mark Butler ame mkosoa kiongozi wa chama cha Nationals kwa kuingilia kati hotuba yake kuhusu matokeo ya afya vijijini wakati wa maswalai namajibu. Mbunge Rebekha Sharkie alimuuliza waziri wa afya, kile ambacho serikali inafanya kuunda usawa wa upatikanaji wa huduma ya afya katika kanda ya Australia. Swali lake lili husiana na utafiti uliofanywa na Muungano wa Kitaifa wa Afya ya Vijijini katika mwaka wa 2023, ambayo ilionesha wa Australia wanao ishi katika maeneo ya vijijini wanapokea $850 kwa kila mtu chini zaidi kwa huduma ya afya kwa wastan kuliko wenzao wanao ishi katika miji mikuu.
Muungano wakitaifa wa Usalama wa wanawake umesema amri zakukabiliana na unyanyasaji wakifamilia zinafeli kuwalinda waathirika wa visa vya ukatili wa nyumbani.
Amri hizo zime undwa kujenga utengano kati ya wahalifu na waathiriwa kwa kutoa fursa za kutembelea ila, muungano huo umesema mara nyingi hazitimizi kusudi hilo. Kati ya miaka ya 2010 na 2018, Shirika lakitaifa la Utafiti kwa usalama wa Wanawake lilipata kuwa amri za unyanyasaji wa nyumbani, zilihusu asilimia 40 za kesi 240 za mauaji yanayo mhusu mpenzi wa karibu.
Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, anasubiriwa kwa hamu kutoa hotuba yake ya kukubali uteuzi wa chama chake cha Democrat kuwania urais wa Marekani kwenye uchaguzi wa Novemba, ambapo atachanjaza maono yake. Kamala Harris ataufunga mkutano mkuu wa Democrat kwa kukubali uteuzi huu wa kihistoria wa kuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika na Asia kuwania nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini Marekani, na kwa wengi kwenye chama chake wanangojea kuona ni jinsi gani atatumia haiba yake ya kuchangamsha, kuwashawishi mamilioni ya wapigakura ambao bado hawajaamuwa kwamba ni yeye anayefaa kumrithi Joe Biden hapo tarehe 4 Novemba.
Kamala, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, ataweka wazi maono yake juu ya Marekani anayotaka kuijenga, na wakati huo huo kujenga hoja dhidi ya mpinzani wake kutoka chama cha Republican, Donald Trump.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, siku ya Jumatano, alitangaza kuwa anaachan na siasa za nchi yake, kutafuta Unyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Uchaguzi huo utafanyika mwezi Februari mwaka 2025, wakati marais wa Afrika watakapokutana jijini Addis Ababa kumchagua kiongozi mpya kuchukua nafasi ya Moussa Faki, ambaye muda wake unafika mwisho. Waziri Mkuu huyo wa zamani ameongeza kuwa, kwa sasa kazi kubwa iliyo mbele yake ni kutafuta nafasi hiyo kwenye Umoja wa Afrika.
Wizara ya afya nchini Burundi imethibitisha visa 171 vya maambukizo ya mpox, taarifa inayokuja baada ya kisa cha kwanza kuripotiwa mwezi uliopita. Zamani ukijulikana kama monkeypox, mpox ni ugonjwa unaambukizwa kwa binadamu kutoka kwa wanyama ambapo pia unasambazwa baina ya binadamu kupitia kutagusana na mtu aliyeambukizwa. Akithibitisha visa hivyo, waziri wa afya Polycarpe Ndayikeza aidha ameeleza kwamba hakuna mgonjwa aliyefariki kutokana na mpox.