Taarifa ya Habari 20 Septemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mswada wa serikali ya shirikisho waku ongeza malipo ya uzeeni katika likizo ya wazazi yenye malipo ime idhinishwa na bunge.


Mswada huo utawaruhusu wazazi wanao stahiki kwa msaada huo, kupokea asimilia 12 ya ziada kwa malipo yao kama mchango kwa malipo yao ya uzeeni. Sheria hiyo mpya inatarajiwa kuwanza kutumika kuanzia Julai 1 2025.

Muswada wa chama cha Labor wa msaada wakununua umecheleweshwa kwa miezi mbili, baada ya mashauriano kati ya chama cha Labor na Greens kukwama. Vyama vya Greens na mseto, vili fanikiwa kuchelewesha rasimu ya muswada huo kwa miezi mbili.
Mfumo wa kusaidia kununua ume ahidi kuwapa wanunuzi wa nyumba ya kwanza elfu 40, upatikanaji wa amana za bei nafuu kupitia mfumo wa usawa na serikali ya shirikisho.

Seneta huru Gerard Rennick amesema kiwango cha kutolipa ushuru kina stahili ongezwa.
Julai mwaka jana, serikali ya shirikisho iliwasilisha makato ya ushuru ambayo, yalipunguza viwango vya ushuru nakuongeza viwango vya wanao lipa ushuru kwa wanao pokea malipo ya kati. Seneta Rennick ameongezea kuwa, mfumo wa sasa wa ushuru una madhara hasi kwa uzalishaji wa Australia.

Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) 19.09.2024 kimetoa ripoti inayothmini hali ya demokrasia nchini Tanzania, ambayo inaonyesha mafanikio na changamoto za hali ya demokrasia katika taifa hilo la Afrika mashariki. Ripoti hiyo inatolewa wakati wadau walioshiriki mjadala wa ripoti hiyo, wakisisitiza maridhiano na amani kama njia kuu ya kuleta suluhu kwa yanayoendelea nchini ikiwamo utekaji, mauaji namadaiya kuminywa demokrasia kwa vyama vya upinzani. Awali, kabla ya ripoti hii kutolewa, Mgeni rasmi katika mjadala huo, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisisitiza maridhiano na majadiliano.

Jeshi la Sudan na kikosi kilichoasi cha RSF, yamesema kuwa yako tayari kwa mazungumzo ya amani na kuvimaliza vita ambavyo vinaendelea kwa zaidi ya miezi 17. Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan alisema siku ya Jumatano kwamba serikali ya nchi hiyo iko tayari kwa juhudi zote zinazolenga kumaliza vita na wako "tayari kufanya kazi na washirika wote wa kimataifa katika kutafuta suluhu ya mzozo ili kupunguza mateso ya raia na kuiweka Sudan kwenye njia ya kuelekea usalama, utulivu, utawala wa sheria na kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia". Hayo ni baada ya wito wa Rais Joe Biden wa kuzitaka pande zote kurejea katika meza ya mazungumzo ya kusitisha mzozo.

Kinara wa muungano wa upinzani wa Lamuka nchini DRC Martin Fayulu amemwambia mkuu wa operesheni za kulinda amani wa UN, Jean-Pierre Lacroix, kuushawishi Umoja wa Mataifa kuunga mkono mpango wake wa mazungumzo ya kitaifa kwa ajili ya upatanisho wa wanakongo. Martin Fayulu aliitoa kauli hiyo hapo jana wakati alipokutana na mkuu huyo wa operesheni za kulinda amani za umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, ambaye yuko ziarani nchini Jamhuri ya kidemokrasiaya Congo, ambako ameendelea kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali nchini humo. Mbali na Fayulu, Jean Pierre Lacroix pia alikutana na waziri wa mambo ya nje wa DRC Thérèse Wamba Wagner ambapo alisema jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa ukaraibu mchakato wa upatikanaji wa amani ya mashariki mwa nchi hiyo.

Share