Mwanaume huyo mwenye miaka 33, amefunguliwa mashtaka kadhaa yanayo jumuisha kuwa na vilipuzi, tisho la uongo lakutengeza bomu, usafirishaji wa mihadarati, kuwa na silaha pamoja nakufaidi kupitia uhalifu na wizi wa gari. Polisi wamedai wamepata vifaa vinavyo shukiwa kuwa vilipuzi pamoja na silaha katika msako walio fanya ndani ya nyumba moja mjini Geelong, baada ya tisho hilo la bomu kutolewa, ambalo wanasema hali husiani na ugaidi.
Serikali ya New South Wales imetetea uamuzi wayo waku wasilisha punguzo la ushuru wa mishahara kwa ma GP, katika zahanati zinazo toa huduma bila kulipisha, pamoja na msamaha kwa madeni ya kodi ambayo hayaja lipwa. Punguzo hilo litakapo wekwa kisheria, lita toa punguzo linalo endelea kwa mishahara yama GP katika zahanati zinazo toa huduma bila malipo kwa viwango vya asilimia 80 katika maeneo ya mji wa Sydney, na juu ya asilimia 70 katika sehemu zingine za jimbo hilo. Madaktari wamesema kodi ya zamani ya mishahara ingelifanya zahanati hizo zisiweze toa huduma na, kuwalazimisha ma GP walipishe wagonjwa takriban $20 wanapo hudumiwa.
Ripoti mpya imedokeza kuwa mfumo wakisheria una wafeli wahamiaji, wanapo jaribu kudai mishahara ambayo haija lipwa.
Chini ya sheria za Haki ya Kazi, wahamiaji wanahaki yakuwajibisha waajiri wao kupitia mahakama ya madai madogo ila, ripoti kutoka Taasisi ya Haki ya Wahamiaji, imepata kuwa ni watu 137 tu kati ya maelfu ambao hawaja lipwa mishahara yao ipaswavyo ndiwo wamejaribu kudai mishahara yao kote nchini katika mwaka wa 2022/2023. Fiona Yeh ni mwandishi mwenza wa ripoti hiyo amesema, haki za wafanyakazi kulipwa inavyo faa chini ya sheria, ni uongo kama hawa wezi tekeleza haki hiyo mahakamani. Ripoti hiyo imependekeza pawe mchakato mpya waku suluhisha migogoro na kurahisisha kushughulikia baadhi ya changamoto zinazo husiana na kuwasilisha madai.
Moja ya vikwazo vikuu kwa wakimbizi wa Sudan kujaribu kujenga maisha mapya nchini Uganda ni lugha. Baadhi ya takriban watu 40,000 ambao wamewasili katika miezi ya karibuni walikuwa na wanajua kiingereza kidogo lakini hakiwasaidii kupata ajira au kuingia kwa urahisi katika jamii za Uganda. Kundi la kuwawezesha wanawake lililoko katikati mwa Uganda linajaribu kubadili hilo. Somo la msingi la Kiingereza, linafundishwa kwa wafanyakazi wa zamani serikali na watoto wao. Wakimbizi haO wanaozungumzza lugha ya Kiarabu kutoka Sudan ambao wana hamu kubwa ya kujifunza Kiingereza ili kurahisisha kipindi chao cha mpito nchini Uganda.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini leo ameapishwa kuanza muhula wa pili madarakani kiasi wiki moja tangu chama chake kuingia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na vyama kadhaa vya upinzani.
HafLa ya taifa ya kumwapisha Ramaphosa imefanyika kwenye mji mkuu wa serikali ya nchi hiyo Pretoria na kuhudhuriwa na viongozi wa mataifa kadhaa ya Afrika. Kiapo cha urais kiliongozwa na Jaji Mkuu wa Afrika Kusini Raymond Zondo mbele ya majengo ya Ikulu ya nchi hiyo. Mfalme Mswati III wa Ufalme wa Eswatini, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Bola Tinubu wa Nigeria na Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe ni miongoni viongozi na wageni mashuhuri waliohudhuria hafla ya kuapishwa Ramaphosa. Baada ya kula kiapo Ramaphosa alipigiwa mizinga 21 ya heshima na kulikuwa vilevile na onesho la ndege za kivita zilizoruka kupita juu ya majengo ya Ikulu.
Katika taarifa za michezo:
Mwanariadha Erriyon Knighton ata endelea kustahiki kukimbia katika majaribio yajayo ya timu ya Olimpiki ya Marekani, licha yavipimo vyake kupatwa na vitu ambavyo vime pigwa marufuku. Jopo la usuluhishi lime amua kuwa uwepo wa trenbolone inayo saidia kuongeza uwezo katika mwili wake, ambayo imedaiwa ilisababishwa na nyama iliyo chafuliwa. Uamuzi huo unamaana kwamba Knighton ata epuka kusimamishwa na ataweza kuwania nafasi katika timu ya wanariadha wa olimpiki wa Marekani. Ila uamuzi huo unaweza katiwa rufaa na kitengo cha uadilifu wa riadha, au shirika la dunia lakupambana na matumuzi ya vitu vyakuongeza nguvu mwilini vilivyo pigwa marufuku.