Bw Bandt ameongezea kuwa chama cha Greens kiko tayari kushirikiana na chama cha Labor kupitisha miswada ya nyumba kwa sharti kuwa chama cha Labor kina nia halisi yaku kabiliana na janga hilo", haswa kwa swala laku dhibiti makato ya kodi kwa wawekezaji matajiri.
Usafiri wa reli wa Sydney Metro umefunguliwa rasmi, takriban muongo mmoja baada ya mradi huo kupendekezwa kwa mara ya kwanza. Mradi huo wenye thamani ya $ bilioni 21, ndiwo mradi mkubwa zaidi wa usafiri nchini Australia. Jo Hayden ni waziri wa usafiri wa New South Wales, alikuwa miongoni mwa abiria walio tumia usafiri huo wa metro, ambao una unganisha kitongoji cha Chatswood ambacho kiko kaskazini magharibi ya mji na kitongoji cha Sydnenham. Safari ya kwanza iliondoka kituoni kabla ya saa kumi na moja alfajiri. Hayley Johnson alikuwa miongoni mwa abiria wa kwanza ndani ya reli hiyo ya metro.
Wanaharakati wa haki za wakimbizi wame wasilisha ombi lao, wakiomba kuondolewa kwa watu 140 katika vizuizi vya uhamiaji ambavyo viko nje ya nchi. Wito huo unafuata kuwasilishwa kwa muswada leo wa Mbunge huru Kylea Tink, wenye lengo lakuweka kikomo kwa kuwekwa kizuizini kwa waomba hifadhi kwa siku 90 na marufuku yakuwafunga watoto. Shirika la Asylum Seeker Resource Centre liliwasilisha ombi ambalo limesma lina saini elfu kumi na moja.
Idadi ya watu walioripotiwa kuwa na ugonjwa wa Mpox nchini Afrika Kusini, imeongezeka na kufika wagonjwa 24 na vifo vitatu vimerekodiwa hadi sasa. Kesi 12 kati ya hizo ziliripotiwa jimboni Gauteng, 11 KwaZulu-Natal, 1 huko Western Cape na tayari watu 19 wameshapona huku wagonjwa wawili wakiendelea kutengwa nyumbani. Msemaji wa wizara ya Afya Foster Mahal amesema serikali imeanza kudhibiti ugonjwa huo kikamilifu, kwa kuongeza uchunguzi mipakani na amekiri kwamba kutakuwa na ongezeko la wagonjwa wa Mpox siku hadi siku nchini Afrika Kusini.
Juhudi za kidiplomasia kumaliza vita vya Israel na Hamas zinaboreshwa na ziara mpya ya Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken huko Mashariki ya Kati. Lakini wakati matumaini ya sitisho la mapigano yakiwa juu, utekelezaji huenda ukathibitisha ukawa na changamoto, wachambuzi wanasema. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amerejea Mashariki ya Kati katika msukumo mpya wa kupatikana kwa sitisho la mapigano katika vita vya Israel na Hamas.
Serikali ya Kenya inapanga kukusanya kiasi cha dola bilioni 1.2 kwa kurejesha baadhi ya kodi ambazo hazikupendwa zilizokuwemo katika mswada wa fedha ambao ulifutwa wakati wa maandamano ya mitaani, waziri wa serikali alisema. Rais William Ruto alionya juu ya upungufu wa fedha baada ya kuamua mwezi Juni kutupilia mbali ongezeko la kodi lililozua utata, baada ya siku ya umwagaji damu jijini Nairobi iliyoshuhudia bunge kuvamiwa na polisi walifyatua risasi za moto kwa waandamanaji. Waziri wa Fedha John Mbadi alikiambia kituo cha binafsi cha Citizen TV siku ya Jumapili kwamba serikali ilifikiria kuhusu hatua 49 za kodi ili kujaribu kukusanya takriban dola bilioni 1.2.
Umoja wa Mataifa unashutumu ghasia "zisizokubalika" ambazo zimekuwa zikifanyika dhidi ya wahudumu wa masuala ya kibinadamu, ambapo 280 kati yao wameuawa duniani kote mwaka 2023, rekodi iliyochochochewa na vita huko Gaza na ambayo iko katika hatari ya kupada mwaka 2024. "Kuhalalisha unyanyasaji dhidi ya wahudumi wa masuala ya kibinadamu na ukosefu wa uwajibikaji ni vitu ambavyo havikubaliki, haukubaliki na ni hatari sana kwa operesheni za kibinadamu kila mahali," ameshutumu Joyce Msuya, kaimu mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Jumatatu hii, Agosti 19, kwenye hafla ya Siku ya Wahudumu wa Masuala ya Kibinadamu Duniani.