Watetezi wa walemavu wamesema walipigwa butwaa jana wakati serikali ilitangaza kuwa inakubali tu mapendekezo kumi na tatu ya ripoti ya tume hiyo yakifalme iliyo toa mapendekezo 222. Jibu la serikali limejiri miezi 10 baada ya ripoti hiyo kutolewa mara ya kwanza na wanaharakati, wamesema serikali imekosa kuzungumzia mageuzi muhimu yanayo hitajika kwa haraka.
Wahalifu themanini wa wahalifu wa unyanyasaji wa nyumbani wanao julikana, wamekamatwa katika jimbo la Kusini Australia, katika oparesheni ya polisi iliyodumu kwa mwezi mmoja ikilenga kuzuia na uingiliaji wamapema. Jeshi la Polisi la Kusini Australia limesema oparesheni hiyo iliwatambua wahalifu wa viwango vya juu wanao julikana, ambao wana tisho kubwa kwa waathiriwa pamoja naku wazuia wahalifu kupitia uingiliaji ulio imarishwa. Misako ya utekelezaji wa amri ya marufuku ya silaha nane ilifanywa, mashtaka 148 yalifunguliwa na amri zakuingilia 22 zilitolewa pamoja na tahadhari yakuvizia.
Tamasha ya 24 ya kila mwaka ya Garama ime anza hii leo Agosti 2, tamasha hiyo itaendelea hadi Jumatatu katika eneo la Kusinimashariki Arnhem Land, Wilaya ya Kaskazini. Tamasha hiyo ni sherehe kubwa zaidi nchini Australia ya utamaduni wa Yolngu, Waziri Mkuu ni miongoni mwa wanao hudhuria tamasha hiyo, kuna wasomi pia, watalaam wa sheria na wafanya biashara. Shirika la Yothu Yindi Foundation limetangaza kuwa tamasha ya Garma ya mwaka huu itajulikana kama 'Gurtha-Wuma Worrk-gu – Fire, Strength and Renewal'. Ila tamasha hiyo inajiri baada ya takwimu za ripoti ya Kufunga pengo, inaonesha ubora wa hatua muhimu kwa waAustralia wa asili, imedorora tangu kushindwa kwa kura ya maoni ya the Voice to Parliament Oktoba mwaka jana.
Polisi nchini Uganda wamethibitisha kupatikana kwa mafuvu 17 ya vichwa vya binadamu yakiwa yamezikwa katika eneo la ibaada. Kwa mujibu wa polisi, mavufu hayo yamegunduliwa na watoto waliokuwa wanateka kuni katika kijiji cha Kabanga karibu na mji wa Mpigi, karibia kilomita 40, sawa na maili 24 kutoka jijini kuu la Kampala. Maofisa wa polisi wanaeleza kwamba walipata taarifa kutoka kwa wakaazi kwamba walipata masanduku ya chuma ikiwa na kile kilichoonekana kuwa mafuvu ya binadamu yakiwa yamezikwa katika eneo la ibaada.
Jumla ya biashara 71 zimeathiriwa na amri ya kufungwa kwa biashara hiyo kulingana na Ofisi ya Biashara ya Jiji la Addis Ababa. Serikali za mitaa takribani mbili nchini Ethiopia zimeagiza kufungwa kwa darzeni za biashara zilizopatikana kupandisha bei ya bidhaa za msingi baada ya Benki Kuu kuelezea kushuka kwa sarafu ya taifa, maafisa walisema leo Alhamisi. Biashara zimejikuta katika bei isiyo ya kawaida ya ongezeko kwenye bidhaa nyingi za chakula. Hifadhi hizo ziliagizwa kabla ya kiwango kipya cha ubadilishaji, alisema Sewnet Ayele, msemaji wa Ofisi ya Biashara ya Jiji la Addis Ababa. Jumla ya biashara 71 zimeathiriwa na amri ya kufungwa kwa biashara hiyo, Sewnet alisema.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uzinduzi rasmi wa safari za Treni ya kisasa ya umeme (SGR) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ambapo wachambuzi wa uchumi nchini humo wamesema treni hiyo itapelekea ukuaji wa biashara na uchumi wa wananchi. Kuzinduliwa kwa safari hizo kunatarajiwa kuleta manufaa mbalimbali katika kukuza biashara na uchumi nchini humo kutokana na treni hiyo kutarajiwa kuongeza ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam na kurahisisha usafirishaji wa mizigo.