Taarifa ya Habari 17 Septemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mwanaume anaye shukiwa kuhusika katika jaribio laku muuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, amefunguliwa mashtaka ya uhalifu wakutumia bunduki.


Mwanaume huyo mwenye miaka 58 anaye itwa Ryan Wesley Routh, amefunguliwa mashtaka ya kiwango cha shirikisho ya uhalifu wa matumizi ya bunduki baada yaku gunduliwa, jana akijificha kando ya uwanja wa mchezo wa Golf wa Bw Trump mjini Florida, kwa takriban masaa 12.

Waziri Mkuu ameshinikiza chama cha Greens kuinge mkono mswada wa makazi wa chama cha Labor, utakapo wasilishwa ndani ya Seneti wiki hii. Hakuna uwezekano wa muswada huo kupitishwa ndani ya Seneti, wakati mseto wa upinzani au Greens ukiwa hau ungi mkono muswada wa Labor wakusaidia kununua, au kujenga kwa ajili yaku kodi nyumba. Mpango huo waku saidia kununua nyumba, uta saidia serikali kukopesha asilimia 40 ya gharama ya nyumba, kwa wanunuaji elfu 40,000 wanao stahiki wakati mpango waku jenga kwa ajili yaku kodi itatoa zawadi kwa wajenzi, kujenga nyumba za bei nafuu zaku kodi.

Wakati huo huo chama cha Greens kimesema chama cha Labor kinahitaji kuja katika meza ya mashuariano kujadili sera hiyo ya makazi. Chama hicho kinataka kufutwa kwa ukopaji kwa ajili yakuwekeza kwa nyumba pamoja nakusimamisha ongezeko za kodi iwapo ita unga mkono muswada huo.

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Demokrasia, wachambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania wameeleza kuwa ushiriki mdogo wa wananchi katika masuala ya demokrasia unadhoofisha maendeleo ya kisiasa na kupunguza uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi pamoja na kukwamisha maendeleo ya taifa. Wemetoa wito kwa serikali na wadau mbalimbali kuuelimisha umma juu ya umuhimu wa kushiriki katika utawala ili kuimarisha misingi ya demokrasia.

Nchi za Mali, Burkina Faso na Niger, hivi karibuni zitazindua rasmi pasi zao za kusafiria za kielektroniki, wakati huu mataifa hayo yakionekana kuendelea kuimarisha zaidi muungano wao mpya baada ya kujiondoa ECOWAS. Hatua hii imetangazwa na kiongozi wa kijeshi wa Mali, kanali Assimi Goita, ambaye amesema hatua hii ni njia mojawapo ya kuoanisha hati za kusafiria katika ukanda huo chini ya muungano wa Alliance of Sahel States (AES), uliondwa baada ya nchi hizo tatu zinazotawaliwa na wanajeshi kuvunja uhusiano na mkoloni wao Ufaransa na kuanzisha uhusiano na Urusi.

Zaidi ya watu 500 wamefariki kufuatia mvua kubwa za mfululizo pamoja na mafuriko yaliyolikumba eneo kubwa la kanda ya Afrika ya Kati na Magharibi. Hayo yameelezwa leo na Umoja wa Mataifa ambao umesema nchini Chad peke yake watu milioni 1 wameathirika kutokana na mafuriko hayo. Ofisi ya uratibu wa masuala ya kiutu ya Umoja wa Mataifa-Ocha imefahamisha kwamba mafuriko yameathiri watu laki 6 zaidi nchini Nigeria na laki tatu nchini Niger. Cameroon, Mali na sehemu za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo pia zinakabiliwa na mafuriko yaliyozifunikia barabara na mashamba pamoja na kuharibu makaazi.

Share