Taarifa ya Habari 17 Juni 2024

City - Swahili.jpg

Waziri wa kwanza wa China Li Qiang amekaribishwa ndani ya bunge la taifa, hiyo ikiwa ni ziara ya kwanza ya waziri wa kwanza wa China katika muda wa miaka 7.


Asubui ilijawa kwa matukio ya sherehe kabla ya mazungumzo ya viongozi kati ya Waziri Mkuu Anthony Albanese na Waziri wa kwanza Li mchana wa leo 17 Juni. Waziri Mkuu ata sisitiza umuhimu waku jadili utofauti na umuhimu wakujenga ushirikiano katika maeneo ya maslahi ya pande zote, wakati wa mikutano yake. Kuna idadi kubwa ya jeshi la polisi nje ya bunge la taifa ambako, waandamanaji wanao pinga nakupenda serikali ya China, wame jumuika kwa ziara ya waziri wa kwana Qiang Li. Kume kuwa rabsha kati ya waandamanaji ila, hakuna mtu ambaye amekamatwa.

Uchunguzi unaendelea baada ya mwanamke mmoja kupigwa risasi na jeshi la polisi mjini Melbourne. Wapelelezi wa kikosi cha uhalifu wenye silaha watachunguza tukio hilo na, kitengo cha viwango vya kitaaluma kitasimamia uchunguzi huo, kulingana na itifaki ya kawaida. Mwanamke huyo aliye kuwa na umri wa miaka 50, anaendelea kusalia hospitalini akiwa na majeraha mabaya katika mapaja yake. Jeshi la polisi la Victoria limesema mwanamke huyo, alipigwa risasi baada yaku elekea kwa maafisa wa polisi katika hali yakutisha akiwa na kisu katika kitongoji cha Thornbury ambacho kiko mjini Melbourne.

Raia wa Malawi walikusanyika kuomboleza kifo cha aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Saulos Klaus Chilima huku kukiwa na ulinzi mkali siku ya Jumatatu.
siku moja baada ya watu kutoka kwenye kijiji chake kuanzisha maandamano kuhusiana na majibu ya serikali kwa ajali ya ndege iliyomuua makamu huyo wa rais na watu wengine wanane. Chilima mwenye umri wa mika 51, amezikwa katika kijiji chake cha Nsipe kilichopo katika wilaya ya Ntcheu, kiasi cha kilometa 160 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Lilongwe.

Baada ya kuchaguliwa kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, kutokana na kura za upinzani, suala la uthabiti wa muungano linaibuka. Inajulikana kwamba Democratic Alliance, chama cha kiliberali, na Inkatha Freedom Party, chama cha kihafidhina cha Wazulu, walichangia kura zao kwa African National Congress (ANC), chama tawala.
Muungano ni jambo zuri na huyu ni mpiga kura wa ANC anayesema hivyo. Ntuthulezo Mhlakaza, hapendi Democratic Alliance, lakini muungano wa vyama hivyo viwili unaweza kuwa chanya. “Chama cha Democratic Alliance kina ajenda hii, ANC wana ajenda nyingine na sasa wanapaswa kutafuta uwiano sahihi. Kila upande lazima aonyeshe unyenyekevu ili kuipeleka nchi mbele." Kutakuwa na maendeleo mradi wahusika watakubali.

Katika michezo:

Bryson DeChambeau amesema anatumai mchezo wa gofu wa wanaume unaweza ungana tena, baada ya ushindi wake wa michuano ya wazi ya Marekani. DeChambeau ameshinda michuano hiyo kwa mara ya pili, ambapo alimshinda Rory McIlroy kwa alama moja tu. Alimaliza mchezo huo akiwa na matokeo ya sita chini ya par kwa ujumla.

Share