Taarifa ya Habari 15 Novemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Australia ime unga mkono azimio la Umoja wa Mataifa, lakutambua mamlaka yakudumu ya watu wa Palestina kwa mara ya kwanza katika miongo mbili.


Australia imejiunga na nchi zingine 158 katika kamati ya umoja wa mataifa kupiga kura ya kuunga mkono azimio lakutambua mamlaka yakudumu yawatu wa Palestina katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Nchi saba zilipiga kura dhidi ya azimio hilo, Marekani, Canada na Israel ziki jumuishwa. Nchi kumi na moja haziku piga kura.

Uchunguzi wa ufisadi kwa ubaguzi wa rangi ndani ya kitengo ch majibu ya kimbinu katika jesi la polisi la wilaya ya kaskazini, ume fungwa bila matokeo mabaya licha ya kukiri kwa ubaguzi waki historia kwa misingi ya rangi.

Uchunguzi wa ufisadi kwa ubaguzi wa rangi ndani ya kitengo ch majibu ya kimbinu katika jesi la polisi la wilaya ya kaskazini, ume fungwa bila matokeo mabaya licha ya kukiri kwa ubaguzi waki historia kwa misingi ya rangi. Uchunguzi huo ulisababishwa na ushahidi kutoka kwa konstebo wa zamani Zachary Rolfe, katika uchunguzi kwa kisa chakupigwa risasi hadi kufa mwanaume mmoja mu Aboriginal kwa jina la Kumanjayi Walker, katika eneo la kusini magharibi ya mji wa Alice Springs mnamo mwaka wa 2019. Tume huru dhidi ya ufisadi ilipata kulikuwa ushahidi wa ubaguzi wa rangi kabla ya 2015 ila, visa hivyo havikuwa katika miaka iliyo fuata.

Wanasiasa watakabiliwa kwa vikomo vya matumizi kwa mara ya kwanza chini ya mageuzi makubwa ya uchaguzi yatakayo wasilishwa bungeni wiki ijayo. Wagombea wataweza pokea tu $20,000 kutoka mfadhili yoyote kila mwaka, kikomo kamili kikiwa $600,000 kwa michango yakisiasa kila mwaka kwa watu binafsi, biashara, vyama vya wafanyakazi na makundi mengine. Ufichuzi wa wakati halisi utaanzishwa na, kikomo kwa ufichuzi kita punguzwa hadi $1000. Mageuzi hayo hayata anza tumika hadi baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Nchini DRC barua ya kwanza imewasilishwa hivi punde siku ya Jumatano kwa Bunge la taifa la kukagua muda wa muhula wa rais na mageuzi ya mahakama ya Kongo. Ni shirika la kiraia lililochukua hatua kwa sababu hii ya kisiasa ambayo inazua hisia ndani ya upinzani, mashirika ya kiraia na Kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini. Chama cha Kitaifa cha Waathiriwa kinadai kukusanya sahihi 100,000, kama inavyotakiwa kisheria, ili kuwasilisha suala hilo kwa mjadala katika Bunge la Kitaifa. Saini zilikusanywa kote nchini, kulingana na shirika hili lisilo la kiserikali linalongozwa na Mhyrhand Mulumba. "Vifungu vingi vya Katiba vinaonekana kupitwa na wakati na haviendani na hali halisi ya sasa ya kidemokrasia," anaeleza.

Nchini Burundi, mwanahabari Sandra Muhoza huenda akafungwa jela miaka 12 kuhusiana na taarifa aliyochapisha kwenye kundi la WhatsApp kwa mujibu wa shirika la wanahabari wasio na mpika RSF. Kwa mujibu wa RSF, mwanahabari huyo amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miezi saba, shirika hilo lilikosowa mashtaka dhidi yake.Muhoza anatuhumiwa kwa kudharau uadilifu wa taifa kulingana na RSF. Katika taarifa yake, shirika hilo linasema mashtaka dhidi ya mwanahabari huyo yanahusishwa na ujumbe ambao aliuchapisha kwenye kundi la WhatsApp kuhusiana na usambazaji wa silaha na serikali.

Mamia ya familia eneo la Riverside katika mtaa wa mabanda wa Soweto, Kayole, Nairobi zinalilia haki baada ya ploti walimoita nyumbani kubomolewa na tingatinga. Waathiriwa, ambao kwa sasa wanalazimika kulala katika vibanda vilivyoezekwa kutumia mifuko ya plastiki na kupikia vyakula nje ya uwanja wanaomba asasi husika za serikali kuchunguza kisa hicho.

Share