Taarifa ya Habari 13 Septemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mdhibiti wa vyombo vya habari nchini, atapewa mamlaka yakuchukua hatua dhidi ya makampuni ya teknolojia kama Meta na X, kwa usambazaji wa habari potofu na habari feki katika mitandao yao.


Tume ya uchaguzi ya Australia (AEC) imethibitisha uamuzi wayo waku ondoa eneo bunge la Kaskazini Sydney. Wapiga kura elfu 97 wa eneo bunge hilo sasa, wame tawanywa katika maeneo bunge tatu ya Kaskazini Sydney ya: Bradfield, eneo bunge la Bennelong ambalo liko chini ya uongozi wa chama cha Labor na eneo bunge la Warringah ambalo mbunge huru ndiye mwakilishi.

Tuki salia katika maswala ya siasa, tuelekee jimboni Queensland ambako kampeni ina endelea kwa kina, na kiongozi wa jimbo hilo Steven Miles ana wasilisha kesi yake kwa wapiga kura jimboni humo. Bw Miles alionekana ni kama anatoa msimamo wake wa mwisho wakati bunge la 57 la Queensland lina fungwa, kabla ya uchaguzi ujao 26 Oktoba 2024. Hali hiyo imejiri wakati chama cha Liberal kime tishia kumaliza utawala wa Labor wa miaka tisa.

Takriban idadi ya wazee milioni 1.4 watapokea msaada wa ziada waku ishi huru nyumbani kabla waingine katika huduma za wazee baada ya serikali ya shirikisho na upinzani, kuafikiana kuhusu mfumo wa msaada wenye thamani ya dola bilioni 5.6 bungeni. Kusaidia kuwekeza ongezeko ya gharama ya huduma, watakao hitaji huduma hiyo itabidi wagharamie michango ya malipo yao.

Zaidi ya wafungwa wanawake 260 walishambuliwa kingono wakati wa jaribio kutoroka gereza kuu la Makala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwezi huu, ripoti ya ndani ya Umoja wa Mataifa iliyoonekana na shirika la habari la Reuters ilieleza. Takriban watu 129 waliuawa wakati walinzi wa gereza walipotumia silaha za moto dhidi ya wafungwa wanaojaribu kutoroka gerezani mjini Kinshasa ambapo takwimu rasmi zinasema lina uwezo wa kuhifadhi wafungwa 1,500 lakini lina wafungwa zaidi ya 15,000.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimetishia kuanzisha maandamano makubwa zaidi, tangazo linalokuja baada ya kutuhumu mamlaka kwenye taifa la Afrika Mashariki kwa kuwauua na kuwateka wanachama wake. Chama cha Chadema hapo jana Jumatano kimetishia kuandaa maandamano hayo katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam tarehe 23 ya mwezi Septemba. Chadema kinasema iwapo serikali haitochukua hatua ya kuchunguza na kueleza walipo wanachama wake waliotoweka basi hakitakuwa na buda bali kuitisha maandamano. Rais Samia ametangaza kupunguza baadhi ya marsharti ambayo upinzani na vyombo vya habari vilikuwa vimeekewa chini ya uongozi wa rais Pombe. Licha ya hayo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yameelezea wasiwasi wake kutokana na oparesheni za hivi karibuni ikiwemo kukamatwa na kuzuiliwa kwa wanachama wa upinzani walipokuwa katika mkutano wa kisiasa mwezi uliopita.

Wafanyakazi wa viwanja vya ndege nchini Kenya wameamua kusitisha mgomo na kurudi kazini baada ya kufikia makubaliano na serikali. Katika makubaliano hayo ya kurudi kazini kwa wafanyakazi hao, serikali itaruhusu uchunguzi wa stakhabadhi kuhusu ukodishaji wa miaka 30 wa uwanja wa ndege wa JKIA na kampuni ya India ya Adani. Gazeti la Nation Daily nchini Kenya, limebaini kwamba vyama vya wafanyakazi kwenye viwanja vya ndege vya JKIA pamoja na vile vya Mombasa na serikali kufuatia mkutano kati ya Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir, Viongozi wa Muungano wa wafanyakazi na katibu wa Muungano wa wafanyakazi nchini Kenya Cotu Francis Atwoli.

Share