Taarifa ya Habari 12 Novemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese ametoa pongezi kwa mkongwe wa vita vya Vietnam Richard Norden, ambaye amepewa tuzo baada ya kufa ya ngazi ya juu zaidi ya jeshi la Australia ya Victoria Cross.


Naibu Kiongozi wa chama cha Greens na msemaji wa elimu, Mehreen Faruqi, amesema kufuta deni ya wanafunzi kuta leta mageuzi halisi katika maisha ya vijana. Chama cha Greens, kina zindua mpango wakufuta deni zote za HECS za wanafunzi wa chuo. Hali hiyo imejiri baada ya serikali ya shirikisho kuweka wazi mpango wayo waku kata deni za wanafunzi kwa asilimia 20, iwapo itashinda uchaguzi mkuu ujao.

Shirika linalo shughulikia Hali ya hewa duniani, lime onya kuhusu hatari kubwa kwa mabadiliko ya mazingira wakati nyuzi joto zina ongezeka duniani kwa viwango vikubwa.
Katika ripoti yake mpya, shirika hilo limesema joto duniani katika mwaka wa 2024 ulifika nyuzi joto 1.5 juu ya viwango vya kabla ya viwanda. Hiyo inafanya mwaka wa 2024 kuwa mwaka wenye joto zaidi kwa sababu ya tukio la El Nino, ambalo lime ongeza joto duniani.

Shirika la ndege lakikanda Rex, limepewa njia ya maisha ya uendeshaji na serikali ya shirikisho ambayo ime lipa $80 milioni kuendeleza oparesheni zake zakikanda. Rex ili ingia katika utawala wa hiari mnamo Julai baada ya ndege zake aina ya Boeing 737 zilizokuwa ziki safiri katika vituo vya miji mikubwa kusimamishwa. Zaidi ya wafanya kazi 600 walio kuwa wame simamishwa kazini, watapewa mafao yao mapema.

Matokeo ya mwisho bado hayajatolewa lakini kiongozi wa upinzani Navin Ramgoolam anaonekana kuwa waziri mkuu kwa mara ya tatu. Waziri Mkuu wa Mauritius Pravind Jugnauth amekubali leo Jumatatu kwamba muungano wake unaelekea katika hali ya kusuasua katika uchaguzi wa bunge unaozozaniwa na kuzusha njia kwa upinzani kuchukua madaraka.

Mamlaka inayohusika na udhibiti wa dawa za kulevya visiwani Zanzibar imezitaifisha mali za raia mmoja wa Kijerumani kwa tuhuma za kuhusika na dawa za kulevya. Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Kanali Burhani Zuberi Nassoro, raia wa Ujerumani kwa jina la Andreas Wolfgang Fretz alikamatwa mwaka jana baada ya kugundulika ameanzisha kilimo cha kisasa cha dawa za kulevya aina ya bangi mseto kusini mwa kisiwa cha Unguja.

Share