Taarifa ya Habari 12 Julai 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Polisi wadai baba ambaye amefunguliwa mashtaka ya mauaji ya watoto wake watatu, inadaiwa walifunga milango kuwazuia watu kuondoka ndani ya nyumba iliyo kuwa iki ungua katika kitongoji cha Lalor Park mjini Sydney.


Mwanaume huyo mwenye miaka 28 hakuwa ndani ya mahakama ya Parramatta ambako kesi yake ilisikizwa, baada yaku achwa bila fahamu kufuatia moto huo na anaendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi hospitalini. Watoto watatu wenye umri wa miaka sita, mbili na tano walifariki katika moto huo Jumapili, wakati wengine wanne wame lazwa hospitalini. Mwanaume huyo amefunguliwa mashtaka tatu ya unyanyasaji wa nyumbani unao husiana na uuaji, pamoja na makosa mengine tano ya jaribio laku uwa. Mashtaka hayo ya jaribio laku uwa, yana wahusu watoto wengine wanne pamoja na mpenzi wake wa miaka 29 wote amboa walipona moto huo.

Kamishna wa polisi wa Wilaya ya Kaskazini amesema amri ya ghafla yakuto toka nje iliyo wekwa kwa mji wa Alice Springs ili isha jana. Kamishna Michael Murphy amesema katika taarifa kuwa amri yakubaki nyumbani kwa masaa 72, ambayo ilipiga marufuku kufika katika maeneo ya kati ya mji kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi na mbili asubui, ita isha saa sita hamsini na tano kwa masaa ya wilaya ya kaskazini, akiongezea kuwa "hapakuwa sababu zozote" zaku ongeza muda wa amri hiyo. Makabiliano mapya katika mji wa Alice Springs yalikuwa yametishia kuongeza muda wa hatua hizo za dharura zilizowekwa Jumatatu 11 Julai, baada ya matukio kadhaa ya vurugu.

Waziri Mkuu wametupilia mbali uvumi kuhusu tarehe ya uchaguzi mkuu wakati anatangaza mgombea wa eneo bunge la Ryan jimobni Queensland. Rebecca Hack alikuwa mwalimu zamani, atajaribu kurejesha eneo bunge hilo chini ya uongozi wa Labor, kwa sasa eneo bunge hilo linawakilishwa na Mbunge Elizabeth Watson-Brown wa chama cha Greens. Labor iliwakilisha eneo bunge hilo kwa mara ya mishwo katika mwaka wa 2001. Tarehe ya uchaguzi mkuu ujao haija tangazwa ila, lazima itangazwe kabla ya katikati ya mwaka wa 2025.

Rais wa Kenya William Ruto amewafuta kazi mawaziri wake wote nan kuahidi kuunda serikali mpya ambayo itakuwa ndogo na yenye ufanisi kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya kupinga kodi kubwa na utawala mbaya. Ruto alisema alichukua uamuzi huo baada ya kuwasikiliza wananchi na kwamba ataunda serikali pana baada ya mashauriano. ya wiki tatu ambapo waandamanaji walivamia bunge tarehe 25 Juni baada ya mswada wa fedha kupitishwa unaopendekeza nyongeza ya kodi. Zaidi ya watu 30 walikufa katika maandamano hayo, ambayo yamebadilika na kuwa shinikizo la kumtaka rais ajiuzulu.

Rwanda inafanya uchaguzi wake wa urais siku ya Jumatatu, uliotangazwa kama marudio ya kura za maoni zilizoshinda mwaka 2017 ambapo rais anayemaliza muda wake anatabiriwa kushinda kwa zaidi ya asilimia 98 ya kura. Akiwa na umri wa miaka 66, Paul Kagame atapambana na wapinzani wawili kama ilivyokuwa miaka saba iliyopita: Franck Habineza, kiongozi wa chama pekee cha upinzani kilichoidhinishwa (chama cha Green Democratic Party), na Philippe Mpayimana, mgombea binafsi. Wawili hao walipata 0.48% na 0.73% ya kura mtawalia. Bw. Kagame ndiye anachukuliwa kama kiogogo wa kuimarika kwa uchumi wa nchi hiyo, bila kumwaga damu baada ya mauaji ya Watutsi mwaka 1994 na leo hii akitolewa na baadhi ya viongozi wa nchi za Magharibi na Afrika kama kielelezo cha maendeleo. Ukuaji wake thabiti (asilimia 7.2 kwa wastani kati ya 2012 na 2022) umeambatana na maendeleo ya miundombinu (barabara, hospitali, n.k.) kuwezesha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Lakini utawala wake pia unakosolewa kwa jukumu lake katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - ambako jeshi lake linashutumiwa na Umoja wa Mataifa kwa kukutoa msaada kwa waasi wa M23 - na ukandamizaji wake dhidi ya sauti za wapinzani.

Mahakama nchini Uganda imemhukumu kijana wa miaka 24 kifungo cha miaka sita jela kwa kumtusi rais na familia yake kupitia video yake iliyowekwa kwenye TikTok. Edward Awebwa alishtakiwa kwa matamshi ya chuki na kueneza taarifa "za kupotosha na zenye nia mbaya" dhidi ya Rais Yoweri Museveni, Mke wa Rais Janet Museveni na mwanawe Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mkuu wa jeshi. Mahakama pia iliarifiwa kwamba Awebwa alikuwa ametoa taarifa za kupotosha - akisema kutakuwa na ongezeko la ushuru chini ya Rais Museveni. Alikiri kuwa na hatia na kuomba msamaha.

Share