Wenye wame elezwa waepuke kugusa maji katika maeneo ya Cherry Creek, Anderson's Swamp na Kayes Drain baada ya vichafuzi vya mazingira kutoka maji ya moto kuingia katika maji hayo. Michelle Carling in mzima moto katika shirika la Fire Rescue Victoria, amesema kemikali tofauti zilikuwa ndani ya kiwanda hicho.
Baba mmoja amefunguliwa mashtaka kwa mauaji ya watoto wake watatu baada yakushtumiwa kwa kuwazuia kuokolewa kutoka nyumba iliyo kuwa iki ungua katika kitongoji cha Lalor Park, mjini Sydney. Mwanaume huyo mwenye miaka 28 atafikishwa katika mahakama ya Parramatta kwa video akiwa katika kitanda chake ndani ya hospitali ya Westmead hii leo Alhamisi, ambako anaendelea kuwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, kufuatia, hali yakukosa fahamu iliyo sababishwa na moto huo. Watoto hao watatu walikuwa na umri wa miaka sita, mbili na miezi tano, walifariki katika moto huo Jumapili. Wengine watatu wame lazwa hospitalini. Mwanaume huyo anakabiliwa kwa makosa tatu ya unyanyasaji wa nyumbani unao husiana na uuaji, pamoja na makosa mengine tano yajaribio laku uwa.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo utasitisha kwa muda mchakato wake wa kuondoka nchini humo. Hata hivyo hakuna tarehe kamili iliyowekwa ya kuanza kwa awamu ijayo baada ya ile ya kwanza kukamilika mwezi Juni. Hayo ni kwa mujibu wa serikali na ujumbe huo. Mnamo Septemba mwaka jana, Rais Felix Tshisekedi aliuomba ujumbe wa MONUSCO kuharakisha utaratibu wa kuwaondoa walinda amani waliopelekwa katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati kutuliza machafuko yanayosababishwa na makundi yenye silaha yanayopigania udhibiti wa maeneo na raslimali. Zenon Mukongo Ngay amesema kuwa awamu ya kwanza ya kuondoka, katika mkoa wa Kivu Kusini, ilikamilika Juni 25. Awali ilitarajiwa kukamilika mwezi Aprili.
Rais wa Kenya William Ruto ametahadharisha kuwa hatua ya kuukataa mswada wa fedha wa mwaka 2024 itakuwa na athari kubwa kwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika kanda ya Afrika Mashariki. Deni kubwa la nchi hiyo linatarajiwa kuongezeka zaidi baada ya maandamano yaliyompelekea Rais Ruto kuufutilia mbali mswada huo. Haya yanafanyika wakati ambapo Kenya imeshushwa katika kiwango kimoja zaidi katika orodha ya mataifa yasiyoweza kukopesheka. Akiwa anakabiliwa na miito ya kujiuzulu, Rais William Ruto amesema kwamba serikali itageukia kuipunguza kwa nusu, nakisi ya bajeti ya dola bilioni 2.7 kisha igeukie kukopa kiasi kitakachosalia bila kusema atakokopa fedha hizo. Kenya kwa sasa ina deni la dola bilioni 80 kutoka kwa mashirika ya ukopeshaji kama Benki ya Dunia, Shirika la fedha Duniani IMF na China. Jinsi utawala wa Ruto utakavyozipata fedha za kulipa deni hilo bila kuwaghadhabisha zaidi Wakenya ambao wanakabiliwa na ugumu wa maisha na bila kuipunguza kasi ya ukuaji wa uchumi, ndilo swali kuu.
England imetinga fainali ya kombe la ulaya baada yaku pata ushindi wa magoli mbili kwa moja dhidi ya Uholanzi mjini Dortmund. Waholanzi walifunga goli mapema katika mechi hiyo kupitia kombora la Xavi Simons ila, penati ya Harry Kane muda mfupi baadae ili ipa England goli laku sawazisha. Na dakika moja kabla ya mechi hiyo kuisha Ollie Watkins alifunga goli la ushindi nakuipa England nafasi yaku kabiliana na Uhispania katika fainali hiyo katika uwanja wa Olympiastadion mjini Berlin Jumapili. Na katika kombe la Copa Amerika, Argentina ita pambana na Colombia katika dimba la Hard Rock Stadium mjini Miami Jumatatu kwa masaa ya Australia.