Taarifa ya Habari 10 Septemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Wauguzi na wakunga kote jimboni New South Wales, wanao ondoka kazini leo Jumanne 10 Septemba, kinyume na amri za tume ya mahusiano ya serikali ya viwanda kusitisha mgomo maramoja.


Jimbo la Queensland lime anza vikao vya elimu kabla ya uzinduzi wa uchunguzi wakusema ukweli na uponyaji baadae mwezi huu. Uchunguzi huo utasikia ushahidi kutoka kwa wazee na wanachama wa jumuiya unapo tafuta nakuchangia historia ya Queensland.

Australia imepiga hatua karibu kupiga marufuku watoto wenye chini ya miaka 14 kutumia mitandao yakijamii. Waziri Mkuu Anthony Albanese hii leo Jumanne itawasilisha muswada mpya, kutekeleza kima cha chini cha miaka kwa matumizi ya mtandao wakijamii. Muswada huo, wenye msingi wake kwa ripoti ya hakimu mkuu wa zamani wa mahakama kuu Robert French, itawasilishwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Wachunguzi wanatazama uwezekano kuwa watoto watatu wachanga walio jeruhiwa katika moto ulio choma nyumba moja mjini Melbourne, walikuwa nyumbani pekee yao.
Watoto hao, ina aminiwa wana chini ya miaka mitano wana endelea kupokea huduma hospitalini kwa majeraha yanayo tishia maisha, kufuatia moto ulio choma nyumba katika kitongoji cha Sydenham usiku wa Jumapili 8 Septemba.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ameviamuru vyombo vya usalama nchini humo kufanya uchunguzi wa matukio ya utekaji nyara na mauaji. Agizo hilo amelitoa saa chache baada ya mwanasiasa wa chama cha upinzani kupatikana akiwa ameuawa. Ali Mohamed Kibao, mjumbe wa kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, alitekwa nyara siku ya Ijumaa na watu waliojitambulisha kuwa maafisa wa polisi akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda mji wa mwambao wa Tanga uliopo kaskazini mashariki mwa Tanzania. Duru zinasema kundi hilo la watu lilisimamisha basi la abiria alimokuwamo Kibao na kumwamuru ateremke na kutokomea naye kusikojulikana. Mwili wake ulipatikana jana Jumapili nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam ukiwa na majeraha ya kipigo na tindikali.

Uchunguzi wa kutumia vinasaba, DNA unatarajiwa kuanza leo nchini Kenya kusaidia kuwatambua wanafunzi waliopoteza maisha katika mkasa wa moto kwenye shule ya Hillside Endarasha katika kaunti ya Nyeri, wiki iliyopita. Watoto hao walifariki dunia siku ya Alhamisi baada ya moto kuteketeza bweni lao katika shule hiyo ya Hillside Endarasha walipokuwa wamelala. Siku ya Jumamosi, msemaji wa serikali Isaac Mwaura, alisema miili 19 ilipatikana kwenye magofu yaliyoteketea ya jengo hilo, huku wanafunzi wengine wawili wakifia hospitalini, na 17 bado hawajulikani waliko.

Shambulizi la kombora katika soko la Sennar kusini mashariki mwa Sudan liliua watu 21 na kujeruhi wengine 67 Jumapili, chanzo cha matibabu kimeiambia AFP, kikilaumu wanamgambo kuhusika na shambulizi hilo. Chama cha madaktari wa Sudan, ambacho kilianzishwa baada ya vita kuanza mwezi Aprili mwaka 2023 kimeripoti idadi hiyo hiyo ya vifo, lakini kimesema idadi ya waliojeruhiwa ni zaidi ya 70. Kimekilaumu kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) kwa kufanya shambulizi hilo la kombora. RSF inayoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo, inapambana na jeshi la Sudan chini ya uongozi wa Abdel Fattah al-Burhan. Serikali hapo awali ilishtumu RSF kwa kulenga raia na taasisi za kiraia.

Share