Taarifa ya habari 1 Oktoba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waangalizi wa watumiaji wa Australia wanatarajiwa kupokea jeki ya dola milioni 30, kuchukua hatua kwa matendo ya kuongeza bei kutoka kwa maduka makubwa na wauzaji reja reja.


Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema anataka onya maduka makubwa kuhusu matendo yao. Amedai hela hizo za ziada zita saidia tume ya ushindani na watumiaji ya Australia, kumaliza uchunguzi mwingi zaidi naku tekeleza sheria.

Huduma zakujibu visa vya moto katika majimbo na wilaya zote, ziko katika hali ya tahadhari baada ya kutoa onyo la umma kwa wakaaji wajiandae kwa msimu mgumu wa moto wa vichaka unao kuja. Onyo hilo limejiri wakati New South Wales, huduma yakuzima moto katika maeneo ya vijijini ime sema mwanzo rasmi wa msimu wa moto wa vichaka una anza leo ((1 Oktoba)). Mamlaka wana wahamasisha wakaaji na jumuiya waandae nyumba zao na familia na wawe na mpango wakuchukua hatua wakati wa moto wa vichaka.

Naibu mkuu wa Hezbollah Sheikh Naim Qassem ametoa hotuba siku ya Jumatatu na kusema wako tayari kwa lolote katika kukabiliana na Israel. Hii ni hotuba ya kwanza tangu shambulio la Israel lilipomuua kiongozi wa kundi hilo Hassan Nasrallah, ambaye bado haijulikani lini atazikwa, baada ya mwili wake kutambuliwa Jumamosi. Naim Qaseem amesema wako tayari kwa lolote hata kwa mapambano ya ardhini na vikosi vya Israel na kwamba wataendeleza mwongozo ulioachwa na Nassrallah katika vita hivyo.

Takwimu mpya zina onesha bei wastan ya nyumba nchini Australia bado ina ongezeka ila, kwa kasi ndogo. Data ya kampuni ya CoreLogic imeonesha kuwa bei za nyumba kitaifa ziliongezeka kwa kiwango cha asilimia 0.4 katika mwezi wa Septemba, kiwango hicho kikiwa ni asilimia 6.7 katika mwaka mzima. Thamani ya nyumba ya kati kitaifa kwa sasa ni zaidi ya dola laki nane elfu saba. Melbourne, Canberra na Hobart zili rekodi kupungua katika miezi mitatu iliyopita wakati thamani mjini Perth iliongezeka kwa asilimia 4.7 katika muda huo.

Mwelekeo kuhusu hatima ya Naibu Rais Rigathi Gachagua utajulikana wiki hii hoja ya kumtimua ikitarajiwa kuwasilishwa bungeni Jumanne. Haya yanajiri huku idadi kubwa ya wabunge kutoka eneo la Mlima Kenya wamemtoroka Naibu Rais wakimsuta kwa kuendeleza siasa za kikabila zinazoweza kuleta migawanyiko nchini. Wanasiasa wa mrengo wa Rais Ruto tayari wanadai hoja ya kumtimua Gachagua imepata uungwaji mkono wa wabunge 300. Kwa upande mwingine, wabunge wandani wa Naibu Rais wanashikilia kuwa jumla ya wabunge 180 wanasimama naye na wameapa kupinga hoja hiyo.

Watu wanne walioshitakiwa kwa kosa la kumbaka na kumuuingilia kinyume cha maumbile binti mmoja wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kifungo cha maisha jela na faini ya shilingi milioni moja kwa kila mmoja. Katika kesi hiyo ya jinai Namba 23476 ya mwaka 2024, MT 140105 Clinton Damas maarufu kama Nyundo, ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari magereza C. 1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson na Amin Lema, wamekutwa na hatiya ya kumbaka na kumuingilia kinyume cha maumbile binti mmoja wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam na hivyo kuhukumiwa kifungo cha maisha jela na faini ya shilingi milioni moja kila mmoja. Kesi hiyo ilivuta hisia za watu wengi hasa kutokana vidio iliyosambaa mtandaoni ikiwaonesha waliokuwa wakituhumiwa kufanya tendo hilo wakiwa hawana wasiwasi wowote. Tukio hilo lilizua hasira kubwa kwa wananchi wakitaka hatua kali za kisheria zichukuliwe.

Share