Taarifa ya Habari 1 Novemba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali imethibitisha kuwa inashikilia mafao ya Medicare ambayo hayaja daiwa yenye thamani yama milioni ya dola, kwa sababu wagonjwa hawajatoa taarifa zao za benki ili wapokee hela hizo.


Waajiri wana omba biashara ziweke mkazo zaidi kwa hatua zaku zuia linapo kuja swala la unyanyasaji wakijinsia katika kongamano kubwa linalo endelea jimboni New South Wales.
Takriban idadi ya waajiri 100 wamekutana na wawakilishi wa serikali, kujadili jinsi yakuzuia unyanyasaji wakijinsia katika sehemu za kazi. Wito huo unafuata uamuzi wa serikali ya New South Wales kuanzisha nguvu kazi yenye lengo laku shughulikia swala hili mwisho wa 2023.

Watetezi wa usalama wa vijana wame hoji kwa nini vyama vyakisiasa vimependekeza umri wa miaka 16 kwa marufuku ya mtandao wakijamii. Wawakilishi kutoka mashirika ya eSafety Youth Council na ReachOut wame zungumza kuhusu Mtandao wakijamii na Jumuiya ya Australia, wakihoji kama utafiti una unga mkono vizuizi vya kuongeza umri.
Wali eleza wabunge kuwa elimu ya mtandaoni na kuwajibisha makampuni ya teknolojia kwa kutoa maudhui hatari, inaweza kuwa mbinu bora.

Mahakama kuu nchini Kenya imeondoa amri iliyokuwa imewekwa kuzuia kuapishwa kwa Prof Kithure Kindiki kama naibu rais wa Kenya. Majaji wamesema kwamba kesi ya Gachagua kupinga kuondolewa ofisini itasikilizwa kuanzia Novemba 7. Imesema kwamba Gachagua ana haki ya kukata rufaa. Mkuu wa watumishi wa uma Felix Kosgei ameunda kamaji ya watu 23 na majina yao yamechaoikwenye gazeti rasmi la serikali. Kamati hiyo ina jukumu la kutayarisha sherehe ya kuapishwa kwa Prof Kithure Kindiki kama naibu rais wa Kenya.

Mahakama moja ya mjini Paris imemuhukumu kifungo cha miaka 27 jela daktari wa zamani nchini Rwanda Eugène Rwamucyo kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. Hukumu hiyo ilitolewa jana kwa Rwamucyo, mwenye umri wa miaka 65, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya kimbari na kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu. Upande wa mashtaka umesema kuwa Rwamucyo pia alishtakiwa kwa kueneza propaganda dhidi ya Watutsi na kusimamia shughuli za kuwazika wahanga katika makaburi ya halaiki. Rwamucyo amesema jukumu lake katika mazishi hayo ya watu wengi lilitokana na motisha ya kudumisha usafi na kukanusha kwamba manusura walizikwa wakiwa hai.

Umoja wa Ulaya, umeamua kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025. Ripoti zinasema, Baraza la Umoja wa Ulaya, limetangaza kuongeza muda wa vikwazo hivyo hadi tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka 2025. Vikwazo hivyo, viliwekewa serikali ya Burundi, wakati huo ikiongozwa na Marehemu Pierre Nkurunziza, kutokana na rekodi mbaya ya haki za binadamu na kuwahangaisha wanasiasa wa upinzani na wanaharakati. Wakati wa uongozi wa Nkurunzinza, aliifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu, na kuzua sintofahamu ya kisiasa nchini humo. Kutoka na thathmini ya Umoja huo wa Ulaya, imebainika kuwa hali ya haki za binadamu imeendelea kuwa mbaya na hakuna mageuzi makubwa ya kisiasa yaliyofanywa na uongozi wa kisasa ili kuondoa vikwazo hivyo.







Share