Sekta ya vyuo yadai wanafunzi wakimataifa wanatumiwa kama "mpira" wakisiasa

University graduates

University graduates, Photo credit should read: Chris Ison/PA Wire Source: Press Association

Vyuo na biashara vina fanya kampeni ya ushawishi dhidi ya sheria zenye utata, kuweka idadi ya wanafunzi wa kimataifa kuanzia mwaka ujao.


Wame sema muswada huo ni "sera iliyo harakishwa" na "ni kifaa chaku badilisha mwelekeo wakisiasa".

Ila, serikali imesema mageuzi yana hitajika kuwazuia watu kutumia viza za wanafunzi kama mlango wa nyuma wakubaki Australia.

Onyo dhidi yakuweka vikomo kwa nafasi za wanafunzi wakimataifa zinasema mageuzi yanaweza hatarisha maelfu ya ajira, pamoja na kukandamiza sana juhudi za utafiti wa vyuo vikuu.

Rasimu ya muswada iliyo tangazwa mnamo Mei na waziri wa elimu Jason Clare, inaweza mpa mamlaka yakuweka idadi ya mwisho ya usajili wa wanafunzi wakimataifa kwa masomo na watoaji.

Wataalam wa sera walikosoa pendekezo hilo waki liita "kichocheo cha machafuko'.

Share