Asilimia kubwa ya waathirika na wahanga wa shambulizi hilo, walikuwa wanachama wa Jumuiya ya Wanyamurenge, kabila lawa Tutsi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Jamii hiyo ya Wanyamurenge ambao walikuwa wakimbizi nchini Burundi, wali lengwa kimakusudi na waasi wa Forces Nationales de Libération (FNL), kundi hilo nila wanagambo waki Hutu ambalo limekuwa liki pigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Burundi.
Bw Moise Nzovu ndiye Rais wa Shirikisho wa Wanyamurenge wanao ishi Australia. Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, alifunguka kuhusu ukosefu wa haki kwa jamaa na marafiki walio uawa nakujeruhiwa katika shambulizi hilo, licha ya miaka ishirini ya kampeni zaku watafutia haki.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.