Mamlaka wame ongeza juhudi kuthibitisha kama ni aina mpya ya kirusi kinacho zua hofu, siku kadhaa baada ya WHO kutangaza dharura ya afya duniani baada ya virusi hivyo kusambaa.
Hakuna kesi mpya ya aina mpya ya mpox, ambayo imeripotiwa nchini Australia kwa sasa. Ila, kume kuwa ongezeko kwa aina ya kirusi ambacho si kikali sana ambacho tayari kiko nchini Australia, kuna kesi 35 zilizo rekodiwa katika siku 15 zilizo pita, katika majimbo kadhaa nchini.
Nias Peng ni mtaalam wa virusi katika shirika la CSIRO, amesema ujio wa virusi hivyo ni sawia na ile hali ya 2022. Mamlaka wa Afya wamesema huu ni wakati waku chukua hatua za haraka, kuzuia historia kujirudia.