Key Points
- The Lunar New Year is a significant cultural holiday celebrated in China and other East Asian countries.
- Sydney Lunar New Year Celebrations is known to be the largest outside Asia.
- The Lunar New Year's Day varies annually, occurring at times in January and at other times in February.
Kuna vipengele vinne kuhusu sherehe za Mwaka Mpya. Huwa zina anza wiki moja kabla kwa sherehe ya Mwaka Mdogo, siku ya ukumbusho na sala, ambayo hufuatwa na siku ya kabla ya Mwaka Mpya, siku yaku ungana nakutoa zawadi.
Dkt Pan Wang, ni mhadhiri mkuu katika masomo yaki China na Asia katika chuo cha New South Wales, amesema sherehe ya msimu wa mchipuko wa mimea hudumu kwa siku kumi na tano hadi wakati wa sherehe ya Taa.
"Mwaka Mpya wa Lunar ni mwanzo wa kalenda ya lunar. Kulingana na mizunguko ya mwezi, inaweza itwa pia Mwaka Mpya waki China au Sherehe ya Mchipuko wa mimea," amesema.
"Huwa ina sherehekewa China na katika nchi zingine za kanda la Mashariki Asia kama Korea, Vietnam, na Japan," Dr Wang ame elezea.
Huwa ina sherehekewa pia Malaysia na Mongolia, pamoja na miongoni mwa nchi ambako wanadiaspora wana ishi duniani.
Mwaka Mpya wa Lunar una historia ya zaidi ya miaka 4,000 kuanzia utawala wa Xia au Shang, Dr Wang ameongezea.
Chinese dancers perform during the Sydney Lunar Festival Media Launch at the Chinese Garden of Friendship in Sydney on February 9, 2021. Source: AAP / AAP Image/Bianca De Marchi
"Fursa yakujifunza kuhusu tamaduni za Kusini-mashariki na Mashariki ya Asia"
Dkt Kai Zhang hufanya kazi na Mradi wa lugha yaki China ya sasa katika shule ya Tamaduni, Historia na Lugha ambayo iko ndani ya Chuo cha Taifa mjini Canberra.
Amesema sherehe za Mwaka Mpya wa Lunar Australia ni fursa nzuri kwa watu kutoka sehemu zote za dunia kujifunza kuhusu tamaduni zaki China, Kusini mashariki Asia na Mashariki ya Asia.
"Ni tukio la kitamaduni lenye historia na tamaduni tajiri, maana ya ishara iliyowekwa ndani," amesema.
Namna yakusherehekea Mwaka Mpya wa Lunar
- Kuweka mapambo.
- Kuchangia chakula cha jioni na familia siku moja kabla ya Mwaka Mpwa.
- Kugawa bahasha nyeupe na zawadi zingine.
- Kuwasha baruti na fataki.
- Kutazama densi za simba na dragon.
"Mwaka Mpya wa Lunar husherehekewa kupitia chakula, kula samaki, dumplings, kujumuika na familia pamoja na marafiki," Dkt Wang ame elezea.
"Rangi nyekundu huzingatiwa kuwa rangi ya bahati. Kwa hiyo unapo ona mapambo mengi ya rangi nyekundu, ni tamaduni pia kwa waChina kuwapa watoto bahasha nyekundu kama namna yaku sherehekea mwaka mpya na kusherehekea ukuaji wao."
Iris Tang alikuwia China na kuhamia Australia miaka 20 iliyopita.
Amesema tofauti kati ya sherehe hizo nchini Australia na China bara, ni kwamba nchini kwao, kuna likizo ndefu ya umma inayo endana na sherehe za mwaka mpya wa Lunar, ni wakati ambapo mamia yama milioni yafamilia huenda katika miji wanako toka nchini China kujumuika na familia zao.
Kulingana na Tang, chakula ni sehemu muhimu ya sherehe za Mwaka Mpya wa Lunar nchini Australia, na China.
"Nili isherehekea na familia yangu pamoja na marafiki wangu hapa Canberra kwa kuandaa chakula kingi. Vile huwa tunafanya niku keti mezani nakutengeza mamia ya chakula aina ya dumplings kuanzia siku moja kabla ya mwaka Mpya. Huwa na pika zaidi ya aina moja ya chakula na naweza kihifadhi ndani ya friji ya baridi sana na tuna vila katika siku za sherehe za mwaka mpya," Bi Tang amesema.
Kalenda yakitamaduni yaki China
Hatakama China yakisasa inatumia kalenda ya Gregorian, kalenda yakitamaduni ya China, hutumiwa kwa upana China na miongoni mwa wa China wanao ishi ng'ambo kwa sababu inajumuisha likizo zakitamaduni, kama Mwaka mpya wa Lunar waki China, sherehe ya Lantern Festival, na sherehe ya Qingming Festival.
Inatoa pia utaratibu wa majina ya tarehe zaki China ndani ya mwaka ambazo watu hutumia kuchagua siku maalum za harusi, mazishi, kuhama au kuanza biashara biashara Dkt Pan Wang ame elezea.
Kalenda yakitamaduni ya China ni lunar-solar. Ina undwa kwa mzunguko wa mwezi na jua, kwa hiyo inazingatia mizunguko ya mwezi duniani na mzunguko wa dunia kwa jua.
"Katika kalenda hii, mwanzo wa mwezi huamuliwa kwa awamu ya mwezi. Kwa hiyo kama katika kalenda nyingi za lunar, miezi zina siku 29 au 30, na mwanzo wa mwaka huamuliwa kwa mwaka wa jua," Dkt Wang amesema.
Aina tofauti ya kalenda yakitamaduni ya China, hutumiwa kote katika ukanda wa Mashariki Asia.
Siku ya mwaka mpya wa Lunar, inaweza kuwa Januari au Februari kila mwaka.
Sherehe ya Taa
Kitamaduni sherehe za mwaka mpya wa Lunar hudumu kwa wiki mbili kutoka siku moja kabla ya mwaka mpya wa Lunar hadi wakati wa sherehe ya Taa, ambayo husherehekewa siku ya kumi na tano ya mwaka wa lunar, amesema Dkt Kai Zhang.
Kulinganana na kalenda yaki China, sherehe ya Taa huendana na siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza.
"Ina itwa sherehe ya Taa kwa sababu kuna hii tamaduni ambapo, familia hutengezea watoto wao taa ndogo, na huwa wanawasha taa hizo nje ya milango yao," amesema.
"Na tukirejea nyuma katika historia, katika utawala wa Tang, kutakuwa matukio makubwa yatakayo andaliwa siku hiyo."
Source: AAP / AAP Image/Jeremy Ng
"Wakati wakutoa heshima kwa mababu."
Dkt Craig Smith ni mhadhiri mkuu katika masomo ya utafsiri (yakichina) katika taasisi ya Asia ambayo iko ndani ya Chuo cha Melbourne.
Ameishi Taiwan na Korea Korea kwa miaka mingi na ana kumbukumbu nyingi nzuri za sherehe za Mwaka Mpya wa Lunar.
Dkt Smith amesema siku ya Mwaka Mpya wa Lunar Korea Kusini, ni wakati wakutoa heshima kwa mababu, hiyo ni tamaduni ambayo jamii zingine huchangia.
"Katika siku ya mwaka mpya, kila mtu huweka nje chakula cha mababu wao walio aga dunia, watu hutoa heshima zao kwao na huwa wanatoa vinywaji kwa ajili yao," Dkt Smith amesema.
"Historia ya maelfu ya miaka."
Dkt Smith amesema vipengele vingi katika sherehe zakitamaduni za mwaka mpya wa Lunar, vina toka katika nchi zingine kuliko China.
Kwa mfano, ni hivyo kwa densi ya simba, kitamaduni densi hiyo hushuhudiwa katika gwaride za mwaka mpya wa Lunar.
"Wasomi wanapo tazama tamaduni ya densi ya simba, huwa wanatazama maelfu ya miaka ya nyuma na, tumejua kwa muda mrefu kuwa tamaduni nyingi, dini, miziki, na sanaa zilikuja China kutoka sehemu tunako ita sasa nchi za Magharibi Asia au Kati ya Asia, haswa katika sehemu ya barabara ya hiriri," Dkt Smith ame elezea.
Kuna uwezekano tamaduni hii ina chimbuko lake nje ya China. Watu wengi wame iunga na tamaduni zaki Persia kwa misingi ya lugha na tathmini zaki historia.
Mwaka wa sayari waki China huanza nakuisha na Mwaka Mpya wa Lunar.
Kila mwaka katika mzunguko wa sayari wa kila miaka 12, unawakilishwa na mnyama, kila moja yazo ikiwa na sifa yake. Kuna Panya, Ng'ombe, Simbamarara, Sungura, Dragon, Nyoka, Farasi, Mbuzi, Nyani, Jogoo, Mbwa na Nguruwe.