Takriban idadi yawa Australia 3,800 wamesajiliwa na serikali kwa ajili yaku ondoka nchini Lebanon.
Serikali ya shirikisho inakabiliana na changamoto mpya yakisheria kwa mfumo wa vizuizi vya uhamiaji. Shirika la Asylum Seeker Resource Centre, lime fungua kesi mpya kwa niaba ya wakimbizi wenye asili ya Sudan Kusini, ikidai kuwa waomba hifadhi wanastahili achiwa huru kutoka vizuizini hali yao ya ukimbizi inapo thibitishwa. Shinikizo hilo lakisheria lililo wasilishwa Ijumaa 4 Oktoba, linafuata uamuzi wa Mahakama ya Kuu katika kesi namba NZYQ, iliyo sababisha wafungwa 150 kuachiwa huru Novemba mwaka jana. Mwanasheria mkuu katika shirika la Asylum Seeker Resource Centre, Hannah Dickinson, amesema fidia ina tafutwa katika kesi hiyo pia, kwa kuwekwa kizuizini kimakosa.
Wakulima jimboni Victoria wamesema wana jiandaa kwa uwezekano wa ujio wa aina mpya ya kirusi cha homa ya ndege. Zaidi ya idadi ya ndege milioni moja zime angamizwa tayari kwa sababu ya mlipuko wa aina ya kirusi cha H7N3 katika shamba saba za ndege na bata jimboni Victoria mwaka huu ila, shirikisho la wakulima wa Victoria limesema wakulima kwa sasa wanajiandaa kwa uwezekano wa ujio wa aina mpya ya kirusi cha H5N1. Aina hiyo mpya ya kirusi kimsingi ina athiri wanyama ila, katika maambukizi 900 miongoni mwa binadam kote duniani zaidi ya nusu ya visa hivyo vilihusu vifo kwa mujibu wa shirika la afya la dunia. Imesababisha pia idadi isiyo ya kawaida ya vifo katika ndege za porini pamoja na ndege zinazo fugwa kote duniani.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini DRC, Jacquemin Shabani amefahamisha umma kuwa wapigambizi wa ndani wanaoshirikiana na kikosi cha wanamaji na SADC wamemwambia kuwa Meli MV Merdi iliyozama Alhamisi ya Oktoba 3, ilipatikana Jumapili hii kwenye kina cha mita 200 kwenye maji ya Ziwa Kivu huko Goma Taarifa hii ilithibitishwa kwa vyombo vya habari na naibu Waziri Mkuu, pia Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Jacquemin Shabani Lukoo punde baada ya kuwasili mjini Goma hapo jana siku ya jumapili. Meli hiyo ya MV Merdi ilizama Alhamisi, Oktoba 3, kwenye maji ya Ziwa Kivu, karibu na bandari ya Kituku, huko Goma, ambapo idadi kamili ya watu waliokufa haijulikani, huku baadhi wakisema ni 34 na wengine zaidi, manusura wakifikia 80, nayo mashirika ya kiraia ya eneo hilo pamoja na kamati ya wahasiriwa ikitangaza kuwa mamia ya watu hawajapatikana.
Wakenya wameshiriki kwenye mdahalo wa kukusanya maoni kuhusu hoja ya kumtimua makamu wao wa rais, Rigathi Gachagua, lakini zoezi hilo liligubikwa na vurugu kwenye baadhi ya maeneo. Zoezi la kukusanya maoni ya raia lililofanyika siku ya Ijumaa (Oktoba 4) lilitazamia kuendelea siku ya pili yake, kwa mujibu wa taarifa ya karani wa bunge la taifa Samuel Njoroge. Hii ni baada ya mahakama kuu mjini Kerugoya kuamuru kuwa Wakenya wote wanapaswa kushiriki kutoa maoni yao kwenye vituo rasmi vya kupigia kura kote nchini.
Uganda inapoteza takriban dola bilioni 2.5 kutokana na ufisadi kila mwaka, sawa na karibu robo ya bajeti yake ya mwaka. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Ofisi inayopambana na ufisadi alipozungumza na shirika la habari la AFP mapema hii leo.
Ufisadi ni tatizo kubwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo linashika nafasi ya 141 kati ya 180 katika ripoti ya kimataifa ya nchi zenye kiwango cha juu cha ufisadi duniani.
Hivi karibuni yaliibuka maandamano nchini Uganda ya kupinga ufisadi na Rais Yoweri Museveni amekuwa akiahidi mara kwa mara kwamba atafanyia kazi kashfa hizo zinazowakabili maafisa wa umma.