Taarifa ya Habari 8 Agosti 2024

City - Swahili.jpg

Wafanyakazi wa huduma ya malezi ya watoto kote nchini Australia, wana tarajiwa kuongezewa mishahara, iwapo sehemu zao za kazi zita kubali kuto ongeza ada kwa zaidi ya asilimia 4.4 katika mwaka ujao.


Nyongeza hiyo ina wekezwa na serikali ya shirikisho na ita wasilishwa katika muda wa miaka mbili, awamu ya kwanza ita tolewa Disemba kwa asilimia kumi, kisha awamu ya pili ita tolewa kwa asilimia tano miezi kumi na mbili baadae. Wafanyakazi wanao lipwa kwa viwango vya tuzo, wata ona ongezeko kwa mishahara yao kwa $150 kwa wiki kufikia Disemba 2025. Akizungumzia hoja hiyo, Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema nyongeza hiyo ina mulika thamani ya wafanyakazi hao. Mwafaka huo wenye thamani ya dola bilioni 3.6, ilifikiwa na Tume ya Haki Kazini ambayo ina fanya uchunguzi kwa kutothaminiwa kwa wafanyakazi wa elimu ya mapema ya watoto, kazi ya malezi, huduma ya malezi ya nyumbani ya walemavu pamoja na kazi zingine za huduma ya jamii.

Kiongozi wa jimbo la Victoria Jacinta Allan ame wasilisha mpango wa serikali yake, kuwekeza $1.5bilioni katika hospitali, kwa ajili yaku saidia kushughulikia swala la mahitaji mengi. Bi Allan amesema serikali yake imekubali pia mapendekezo 26 kati ya 27 kutoka kwa jopo la washauri watalaam, ambao walifanyia tathmini mfumo wa huduma wa afya wa jimbo hilo. Ameongezea kuwa serikali yake imetupilia mbali pendekezo laku unganisha huduma 76 za afya nabadala yake kuwa na mitandao 11, akisisitiza kuwa kulazimisha hospitali kuunganishwa kuta leta usumbufu kwa wagonjwa na wafanyakazi. Bi Allan aliongezea pia kuwa uwekezaji wa ziada, utasaidia kupiga jeki huduma za afya za jimbo hilo. 

Katika taarifa za kimataifa, maandamano yana endelea Uingereza ambako, maelfu ya watu wame jumuika kupinga maandamano ya watu wa mrengo wakulia wanao lenga vituo vya wahamiaji na ofisi za wanasheria wa uhamiaji.
Maandamano ya vurugu ghasia zilianza wiki jana, baada ya wasichana watatu wachanga kuuawa katika shambulio la kisu karibu ya mji wa Liverpool. Machafuko hayo yame chochewa na taarifa potofu, wakati taarifa za uongo zili sambaa kuwa mshambuliaji husika alikuwa ni muhamiaji muislamu. Huo ni mlipuko mubaya zaidi wa vurugu nchini Uingereza kwa zaidi ya muongo.

Nchini Marekani, Naibu Rais Kamala Harris na mshiriki wake gavana Tim Walz wa Minnesota, wame zindua kampeni yao ya pamoja katika jimbo la Wisconsin. Wawili hao walifanya kampeni katika mji wa Eau Claire, ambao ni lengo muhimu la chama cha Democrats ambao uko takriban kilomita 130 na mji wa St Paul ambako Bw Walz ana ishi. Bw Walz alipigia debe mahusiano kati ya majimbo hayo mawili ya ukanda wa magharibi.

Nchini Kenya, vijana wanaofahamika kama Gen Z wamepanga kuandamana leo dhidi ya rais William Ruto na serikali yake, wakimshtumu kwa kushindwa kupambana na rushwa, uongozi mbaya, ukosefu wa ajira miongoni mwa mambo mengine.
Polisi wamewaonya waandamanaji kutovunja sheria kwenye maandamano hayo ambayo vijana hao wamesema yatakuwa ya mwisho ya kutaka kumwondoa Ruto madarakani. Maandamano hayo ambayo yamepewa jina la nane nane, ni mwendelezo wa yale yalioanza mwezi Juni na July kutokana na muswada wa fedha wa mwaka wa 2024 ambao hata hivyo ulitupiliwa mbali.
Rais Ruto kwa upande wake, amesema ni nchi ya kidemokrasia na hataki fujo.

Mchezaji wa hockey wa Australia Tom Craig atapoteza haki zake zote zinazo salia za olimpiki, baada yaku kamatwa mjini Paris kwa kununua Cocaine. Mwanaume huyo mwenye miaka 28 ali zuiliwa katika kituo kimoja cha polisi mjini Paris Jumanne ila, aliachiliwa bila kufunguliwa mashtaka.
Ameomba radhi timu yake na nchi yake.


Share