Taarifa ya habari 25 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Baadhi ya wabunge huru wanataka makaazi yawekwe kuwa haki ya msingi ya binadamu nchini Australia.


Wabunge hao wamesema serikali inahitaji karabati mfumo ma makaazi ulio vunjika nchini, ambako maelfu yawatu wame athiriwa kwa ukosefu wa nyumba. Wakati huo huo, kodi za nyumba zinazo endelea kuongezeka zime weka miji mbili mikubwa ya Australia miongoni mwa orodha ya maeneo yasiyo faa kuishi duniani kwa sababu ya gharama kubwa.

Data mpya imefichua ongezeko katika idadi ya madaktari, wauguzi na wataalam wa afya kutoka ng'ambo wanao fanya kazi katika mfumo wa afya wa Australia. Ila vikundi vya matibabu vimesema maelfu ya wahitimu wa matibabu wakimataifa, wanapitia wakati mgumu kupata sifa zao kutambuliwa, mamia kati yao wakiwa wamefungiwa nje ya nguvu kazi.

Chama cha wauguzi na wakunga umeweka wazi kuwa kunaweza kuwa ongezeko kubw la mishahara kwa wauguzi wa New South Wales, bila kuumiza bajeti ya jimbo kwa kutumia mabilioni ya dola ya fedha za shirikisho ambazo hazijatumika. Ripoti iliyo fanyiwa uchunguzi na kampuni ya Deloitte nakutolewa na chama cha Wauguzi na wakunga wa NSW jana jumatatu 24 Juni, imeonesha kuwa ripoti ya hospitali isiyo sahihi na isiyofaa imezuia upatikanaji wa uwekezaji wa serikali ya madola wenye thamani ya dola bilioni 3 katika muda wa miaka mitano.

Serikali ya Kenya imesema itaruhusu maandamano yaliyopangwa ya kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha nchini kote yaliyopangwa kufanyika kesho Jumanne, Juni 25 kuendelea mradi tu yawe ya amani. Katika hatua ambayo ni nadra, Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki alisema Jumatatu kwamba wale wanaotaka kuandamana wanaweza kuendelea na mipango yao kwa sharti la kuzingatia sheria. Maandamano hayo yaliyoanza wiki jana yanapinga Mswada wa Fedha wa 2024 unaopendekezwa ambao wanasema ni wa kibabe na utawatwika Wakenya mzigo zaidi wa ushuru.

Mkanyagano ulisababisha mtu mmoja kufariki na wengine 37 kujeruhiwa siku ya Jumapili huko Rubavu kaskazini-magharibi mwa Rwanda wakati wa mkutano wa chama cha Rais Kagame, wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais ambapo anaonekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda uchauzi huo, shirika la habari la Rwanda limeripoti. Siku moja kabla, Paul Kagame, ambaye ametawala nchi hii ya kanda ya Afrika ya Maziwa Makuu kwa miaka 24 kwa mkono wa chuma, alifanya mkutano wa kwanza katika wilaya ya Musenze (kaskazini-magharibi) katika uwanja uliojaa maelfu ya watu wanaomuunga mkono kwa ufunguzi wa kampeni. Mbele ya umati, wengi wao walioletwa kwa basi, Bw. Kagame alitetea rekodi ya "demokrasia" nchini Rwanda, akionekana kujibu ukosoaji wa ukandamizaji wa upinzani. Wapiga kura milioni tisa wamesajiliwa kwa uchaguzi wa urais, kwa mara ya kwanza pamoja na uhaguzi wa wabunge.

Wafanyabiashara katika soko la kariakoo nchini Tanzania wamefanya mgomo na kufunga maduka wakipinga mrundikano wa kodi. Ikiwa si mara ya kwanza kwa wakazi wa Dar es Salaam kushuhudia mgomo wa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo. Mmoja wa wafanyabiashara hao Beatrice John ameiambia sauti ya Amerika, “Mimi nilikuwa ni machinga nilikuwa nanauza bidhaa zangu chini lakini machinga tulifukuzwa barabarani nikaamua kuchukua mkopo nikafungua biashara yangu hii,”





Share