Viongozi wa shule katika jimbo la New South Wales, wakubaliana kwa sauti moja na uongozi wa jimbo hilo kupiga marufuku matumizi ya simu za rununu shuleni.
Kamati ya Seneti yapokea mawasilisho kuhusu muswada mpya wa huduma ya wazee, imesikiza maoni kuwa kutoa muda wa saa moja kwa wiki kwa shughuli za usaidizi hautoshi kuwahudumia wazee ipaswavyo.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa wiki kadhaa yamevunjika baada ya kuanza mapigano mapya katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali.
Naibu Rais aliyeondolewa mamlakani nchini Kenya Rigathi Gachagua, Jumapili alimshamblia mkuu wake William Ruto akisema ni “mbaya sana” na mkatili, akionya kuwa maisha yake yanaweza kuwa hatarini.
Watu wasiojulikana walimteka nyara, kumpiga na kumjeruhi vibaya afisa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema kabla ya kumtupa msituni, chama chake kilisema siku ya Jumapili, mwezi mmoja baada ya kutekwa nyara na kuuawa kwa kiongozi mwingine wa chama hicho.