Taarifa ya Habari 21 Juni 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Australia ime ahidi kuendelea kuwasaidia wakaaji wa Papua New Guinea ambao wanapitia wakati mgumu kumudu maisha baada ya kukabiliwa kwa maporomoko mabaya ya ardhi mnamo Mei.


Waziri wa maswala ya kigeni Penny Wong, waziri wa kanda la Pasifiki Pat Conroy, na Naibu Waziri Mkuu Richard Marles wali toa ahadi hiyo walipo tembelea sehemu ambako maporomoko hayo ya ardhi yalitokea. Seneta Wong ali waeleza wanavijiji hao kuwa Australia inatoa dola milioni 2.2 za ziada ambazo zita saidia kukarabati barabara zilizo athiriwa vibaya pamoja na kuunga jumuiya ambazo zime tengwa tangu tukio hilo la maporomoko ya ardhi.

Wazuru Mkuu ametupilia mbali wasiwasi kuhusu uwezekano wa uhaba wa gesi, katika pwani ya kusini katika miezi ijayo. Opareta wa Soko la Nishati la Australia amesema kunaweza kuwa uwezekano wa upungufu katika orodha za uhifadhi wa kusini kwa sababu, ya mahitaji mengi ya gesi katika miezi ya hivi karibuni ya baridi pamoja na kukatika kwa kiwanda jimboni Victoria. Anthony Albanese amesema ripoti ya AEMO haija mpa wasiwasi wowote na serikali itashirikiana nayo katika utoaji wa gesi ila, kiongozi wa upinzani Peter Dutton amesema onyo hilo ni kumbusho kwa mahitaji ya aina zingine za nishati katika gridi ya taifa.

Mu Australia mmoja yuko miongoni mwa mamia ya watu walio fariki wakati wa Hija nchini Saudi Arabia, kwa sababu ya viwango vya juu joto. Idara ya Maswala yakigeni imethibitisha inatoa msaada waubalozi kwa familia ya mhusika ila, haija weza kutoa taarifa ya ziada kwa sababu ya majukumu ya faragha. Takriban watu 550 wamekadiriwa walikufa katika hija hiyo ya siku tano, baada ya nyuzi joto kufika 47 mjini Mecca na katika sehemu zingine takatifu mjini humo.

Baada ya miezi kadhaa ya kuonyesha hasira kwenye mitandao ya kijamii, maelfu ya Wakenya walikusanyika jijini Nairobi na kwingineko wiki hii kupinga mswada utakaoongeza ushuru ili kulipia mikopo na maendeleo. Maandamano yaliyoanza Jumanne yameendelea kwa siku ya tatu, licha ya serikali kuondoa sehemu ya mapendekezo ya nyongeza ya ushuru. Jijini Nairobi, mamia ya waandamanaji walijitokeza wiki hii, wakiwataka wabunge kukataa muswada wa fedha wa 2024, ambao unaongeza ushuru katika sekta mbalimbali za uchumi. Baadhi ya kodi hizo za juu ni matokeo ya deni la miundombinu kutoka China. Mamia zaidi waliandamana katika mji alikozaliwa Rais William Ruto wa Eldoret, na miji ya Nyeri, Nakuru, Kisii, Kisumu na Mombasa.

Serikali ya Somalia inashinikiza kupunguzwa kwa kasi ya kuondoka kwa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Afrika nchini mwake, ikionya kuhusu uwezekano wa ombwe la usalama, kwa mujibu wa nyaraka zinazoonekana na shirika la habari la Reuters.
Hayo yanajiri huku nchi jirani na Somalia, zikiwa na wasiwasi kwamba wanamgambo wa al-Shabaab, wanaweza kunyakua mamlaka. Kikosi cha Mpito cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS), , kinatarajiwa kuondoka ifikapo Desemba 31, huku kikosi kingine kidogo kikitarajiwa kuchukua nafasi yake.

Serikali ya Tanzania imeelezea msimamo wake kuhusu hatima ya watu wenye ualbino, ambapo imeandaa mikakati maalumu ya kuwalinda watu wenye ualbino inayoanza kutekelezwa mara moja. Tamko hilo limetolewa kufuatia mauaji ya hivi karibuni ya mtoto mwenye ualbino Asimwe Novart ambaye mwili wake uliokotwa mkoani Kagera huku baadhi ya viungo vyake vikiwa vimenyofolewa. Hayo yanajiri wakati ambapo jeshi la polisi nchini humo likitangaza kuwa limewakamata watu tisa wanaotuhumiwa kwa mauji ya mtoto huyo. Akizungumza bungeni mjini Dodoma, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hatua ya kuwalinda watu wenye ualbino ni jambo linalopaswa kutelelezwa na makundi yote ya jamii na kwa upande wake serikali imeweka hatua kadhaa ambazo utekelezaji wake utahusisha wakuu wa mikoa, wilaya, vyombo vya dola, viongozi wa dini pamoja na watoa tiba za jadi.

Share