Taarifa ya Habari 18 Oktoba 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya Shirikisho ya tetea takwimu zake za utoaji wa ajira milioni moja, wakati upinzani una sisitiza kuwa asilimia kubwa ya ajira hizo zime fadhiliwa na serikali ya shirikisho.


Mfalme Charles na Malkia Camilla, wanatarajiwa kuanza ziara ya siku tano nchini Australia. Na data mpya ime pata kuwa viwango vya upangaji kitaifa, vime pungua kwa mwezi wa tatu mfululizo.

Maseneta nchini Kenya wamepiga kura ya kumtimua mamlakani Naibu Rais Rigathi Gachagua, miaka miwili pekee tangu asaidie kuunda serikali ya Kenya Kwanza. Kisheria, kiongozi anahitajika tu kupatikana na hatia ya kosa moja kwake, ili atangazwe kwamba ameng’atuliwa uongozini. Bw Gachagua alipatwa na hatia tano kati ya mashtaka kumi na moja.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ilitangaza siku ya Jumatatu Oktoba 14 kuanzisa tena uchunguzi wake nchii Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Uchunguzi wa uhalifu mkubwa - unaotokana na Mkataba wa Roma - mashariki mwa nchi. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumatatu Oktoba 14, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu alitangaza "kuanzisha upya" uchunguzi wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mapigano kati ya vikosi vya shirikisho vya Ethiopia na wanamgambo kaskazini magharibi mwa nchini humo yanawaweka katika hatari kubwa wakimbizi wa vita kutoka Sudan.Haya yamesemwa na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, lenye makao yake huko New York, Marekani. Shirika hilo limesema limetuma matokeo yake ya awali ya ripoti hiyo kwa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Ethiopia lililokiri kwamba kambi ziko karibu na maeneo yenye machafuko ila ikadai kuna usalama wa kutosha.

Share